Ticker

6/recent/ticker-posts

Tanzania yachapa Somalia 1-0 Chan
Tanzania imeibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Somalia katika mchezo wa kuwania tiketi ya fainali za ubingwa wa Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) mwakani nchini Algeria.

Goli la Tanzania limefungwa na Abdul Sopu dakika ya 46, na hivyo kuiweka Tanzania kwenye nafasi nzuri kuelekea mchezo wa marudiano utakaopigwa kati ya Julai 29 na 31 mwaka huu ambapo mshindi wa jumla atasonga mbele kwenye mechi za mchujo zitakazofikia tamati Septemba 2, mwaka huu.

Fainali za CHAN zilikuwa zifanyike Julai 10 hadi Agosti 1, mwaka huu lakini Shirikisho la Soka Afrika (CAF) likasogeza hadi mwakani kutokana na kuahirishwa kwa fainali zilizopita kusogezwa mbele sababu ya janga la UVIKO19.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments