Ticker

6/recent/ticker-posts

Tarimba Aitaja Simba Kwa Hili Wakati Sports Pesa Wakisaini Mkataba na Yanga

 


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa SportPesa Tarimba Abbas Tarimba amesema Kampuni ya Sportpesa ndiyo Kampuni pekee ya michezo ya kubashiri iliyosaidia kwa kiasi kikubwa kusaidia vilabu vya Simba SC na Young Africans kujiimarisha kiuchumi kupitia udhamini wao lakini pia kupitia mashindano ya Sportpesa tangu mwaka 2017.

Tarimba amesema hayo wakati wa hafla ya kusaini mkataba mpya na Klabu ya Young Africans leo Jumatano (Julai 27) jijini Dar es salaam.


Kuhusu Mkataba mpya, Kiongozi huyo wa SportPesa amesema, Klabu ya Young Africans itanufaika na Mkataba huu kwenye vipengele kadhaa ikiwemo endapo Klabu hiyo itashinda taji la Ligi Kuu ya NBC basi itafanikiwa kunyakua kitita cha Shilingi milioni 150.


Amesema Klabu hiyo pia itafanikiwa kunyakua kiasi cha shilingi milioni 75 endapo tu itafanikiwa kufika fainali ya Kombe la Shirikisho ‘ASFC’.


Kwa upande mwingine Rais wa Young Africans Injinia Hersi Said ameipongeza Kampuni ya Sportpesa chini ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Abbas Tarimba kwa kufikia makubaliano hayo ya kihistoria kwa klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Twiga na Jangwani.


Hersi ameahidi kusimamia maelekezo na makubaliano ya mkataba huo na kusisitiza kuwa Young Africans ipo tayari kufanya mambo makubwa zaidi na Kampuni ya SportPesa.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments