Uwoya Adai Kama Kuna Mtu Anaumizwa na Mapenzi Basi Aende Akalime

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



MUIGIZAJI mrembo wa Bongo Movies, Irene Uwoya amekuja na jipya baada ya kudai kwamba watu wengi katika karne hii ya sasa wanateseka na mapenzi na hivyo akawataka wote walioshindwa na mapenzi basi wajaribu bahati yao katika kilimo, pengine huko ndiko bahati yao ipo.


Uwoya amedai kuwa, haina haja mtu kujiingiza kwenye mapenzi wakati matokeo yake ni maumivu kutwa kucha, wakati furaha yako iko kwenye kilimo huku akiongeza kuwa atakayefuata ushauri wake basi atamshukuru mbeleni.

“Ukishindwa na mapenzi jaribu kilimo ndugu yangu …utanishukuru baadae,” aliandika Uwoya kwenye Instagram yake.


Maneno hayo ya Uwoya yalipokelewa kwa mitazamo tofauti huku baadhi wakisema kwamba kuna waliojaribu vyote na tayari wameshindwa na kutaka ushauri zaidi kupewa jaribio la fani ya tatu mbali na kilimo na mapenzi.


“Nimeshajaribu vyote nimeshindwa sasa hivi sijui nifanyeje?” mmoja kwa jina Dullah Tameer aliandika.

Muigizaji huyo mkongwe ambaye pia ni mama wa mtoto mmoja, baadhi ya mashabiki walitumia kigezo hiki kumuuliza kwa kuwa yeye ametendwa sana katika mapenzi ana mashamba mangapi iwapo aliamua kujaribu kilimo.

“Una mashamba mangapi mpaka sasa? Maana wewe ni mfano hai wa waliokucheka kwenye mapenzi,” mwingine alitoa maoni.

Uwoya katika siku za hivi karibuni ameonekana kutolea ushauri komavu kwa mashabiki zake tangu miezi michache iliyopita.


Hivi karibuni alialikwa kwenye sherehe ya kanisa kama mgeni maalum katika ibada ya kusherehekea miaka minane tangu kanisa hilo lililopo mjini Morogoro kuanza kutoa huduma ya uponyaji na mahubiri.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad