Biden: Hatimaye Haki Imepatikana Baada ya Kumuua Gaidi wa Al Qaeda

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

RAIS wa Marekani Joe Biden amelihutubia Taifa hilo na kutoa kauli nzito juu ya kifo cha kiongozi wa kundi la kigaidi la Al Qaeda Ayman al-Zawahiri, aliyeuawa na ndege ya Marekani isiyokuwa na Rubani.


Rais Biden amesema kuwa kifo cha al- Zawahiri ni malipo ya unyama alioufanya kwa wananchi wa Taifa hilo kufuatia kuhusika katika utekelezaji wa shambuliola kigaidi la Septemba 11 mwaka 2001 ambalo liliua zaidi ya raia 3000 nchini humo.


“Kiongoz wa ugaidi hayupo tena.” Alinukuliwa akisema Rais Biden ambaye aliendelea kwa kusisitiza kuwa kifo cha gaidi huyo kinarudisha tena faraja kwa familia za wahanga wa shambulio la Septemba 11.


Rais huyo wa Marekani amesisitiza kuwa Afghanistan haitakuwa tena makazi ya ugaidi baada ya shambulio hilo kutekelezwa ikiwa ni mwaka mmoja tangu vikosi vya Marekani vindoke nchini humo.


Aidha kiongozi huyo wa kundi la kigaidi ambaye ana asili ya Misri aliuawa majira ya asubuhi wakati akiwa katika nyumba yake kwenye mji wa Kabul ambapo kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Rais Biden ni kwamba hakuna mtu mwingine yeyote yule kutoka katika familia ya al- Zawahiri aliyeathirika au kujeruhiwa katika shambulio hilo.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad