Kinasa Msukuma Atoa ya Moyoni Baada ya kushushwa Stejini na Diamond Platnumz

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Mfanyabiashara maarufu Kinasa msukuma akiwa kwenye steji pamoja na nyota Diamond Platnumz pamoja na Barnaba Classic

SIKU ya Jumanne Agosti 16 katika ukumbi wa Mlimani City kulifanyika uzinduzi wa albamu ya mmoja wa wasanii wakongwe katika tasnia ya muziki wa bongo fleva, Barnaba Classic.

Moja ya tukio liliyozungumzwa sana na mashabiki wa muziki kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ni ile video iliyomuonesha Kinasa Msukuma akiwatunza fedha nyingi Diamond Platnumz na Barnaba wakiwa wanapafomu stejini ambapo alishushwa na baunsa wa Diamond muda mchache baada ya kuanza kufanya hivyo.

Katika kipindi cha katambuga kinachorushwa na Global TV na 255Global Radio Kinasamsukuma amefunguka mengi juu ya tukio lile lilioibua hisia za mashabiki walio wengi.

Kinasamsukuma amesema changamoto iliyotolewa imeshatatuliwa tayari kama mwanafamilia wa WCB

Kinasa anaeleza kusikitishwa na kitendo kile cha kushushwa stejini wakati anatunza pesa kwani alipanda pale baada ya kutajwa mara kadhaa na Barnaba ambaye anamuelezea kuwa ni ndugu yake na alimtaja jina ili aende kutoa sapoti na ndio maana Barnaba alienda kumfokea baunsa wa Diamond baada ya yeye kushushwa stejini.

Hata hivyo anaendelea kusema suala lile wameshalimaliza kama wanafamilia wa WCB ambapo jana alipokea simu kutoka kwa mwanafamilia na mume wa mama Diamond, Anko Shamte kumshukuru kwa sapoti anayoionesha kwao na kumuomba wayamalize yale yote yaliyojitokeza pale Mlimani City wakati wa uzinduzi kwani wao ni wanafamilia na hawana haja ya kutofautiana.

Aidha tajiri huyo kijana ameelezea matamanio yake ya kusaidia kina mama wajane na wale wanaoishi kwenye mazingira magumu kwakuwa anaona ni kundi lililosahaulika katika jamii na linahitaji msaada na amepanga kufanya yote mara baada ya kumaliza kufungua Kampuni yake ambayo ipo kwenye hatua za mwisho kukamilika.

Imeandaliwa na Simon J. Molanga

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad