Ticker

6/recent/ticker-posts

Kuizuia Nyota ya Zuchu Kung'ara Haiwezekani Tena, Aweka Rekodi Mpya Afrika


Kuizuia nyota ya  Zuchu ni sawa na kuziba mwanga kwa kiganja cha mkono. Mwimbaji huyo wa Bongofleva toka WCB Wasafi, ameweka historia ya kuwa msanii wa kike katika nchi zilizopo chini ya Jangwa la Sahara barani Afrika kuwa na subscribers wengi katika mtandao wa YouTube.


Zuchu ambaye alitoka kimuziki miaka miwili iliyopita, amefikisha subscribers Millioni 2.1, nafasi ambayo amempiku msanii toka Nigeria, Yemi Alade mwenye subscribers Millioni 2 ambaye alikuwa anashikilia. Kwasasa nafasi hiyo inashikiliwa na Mtanzania, ZUCHU


Kweye top 10 ya orodha hiyo, nafasi ya kwanza ni Zuchu, kisha anafuata Yemi Alade huku nafasi ya sita ikishikiliwa na Mtanzania, mwimbaji Nandy akiwa na subscribers Millioni 1.7


Zuchu ame-share rekodi yake hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ametoa pia pongezi kwa wanawake wengine kuwepo kwenye orodha hiyo.


Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments