Ticker

6/recent/ticker-posts

Mwanamuziki Mayunga Aiponda Mikataba ya Sony Music na Universal Music Wanayopewa Wanamuziki wa Kibongo


Msanii wa Bongo Flava, Mayunga ambaye kwasasa anafanya poa na wimbo wa DUYUWANNA na Frida Amani, amegusia namna alivyo achana na Label ya Universal Music na kuamua kupush kazi zake mwenyewe. Akiwa kwenye Empire ya EFM, ameeleza kuwa mkataba haukuwa rafiki kwenye kazi zake, hivyo aka9na ni bora hauvunje.


Lakini pia ameelezea sababu zinazo pelekea wasanii wengi kuilalamikia mikataba, ni kutokuwa makini kwenye makubaliano ya mwanzo, mwisho wa siku msanii anakua, value yake inaongezeka zaidi lakini inaendelea kumbana sababu mkataba haubadiliki, upo vile vile toka ausaini akiwa underground hadi anapokuwa mkubwa. Hata kwa upande wake ameelezea kuwa kuna msanii alimtonya kuwa mikataba mikubwa ya Universal/Sony Music kwa Afrika ni majanga, na ndio maana akina Davido waliitema, ila isingekuwa rahisi kumuelewa msanii huyo kwa wakati ule, akijitazama katokea from nowhere hadi kwenye label kubwa duniani.


Mayunga alikuwa ni mshindi wa mashindano ya Airtel Trace Music Star March 30, 2015 na kupata nafasi ya kufanya ngoma na Akon, inayoitwa Please Don't Go lakini kusainiwa kwenye Record label ya Universal Music.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments