Breaking: Mchezaji Mzungu wa Simba Avunja Mkataba"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



ALIYEKUWA Mshambuliaji wa Simba Mserbia, Dejan Georgijevic amethibitisha kuvunja mkataba na miamba hiyo ikiwa ni muda mfupi tangu alipojiunga nao.

Nyota huyo aliyesajiliwa na Kocha Zoran Maki ambaye naye aliondoka na kutimkia Misri alijiunga na Simba Agosti 7 mwaka huu akitokea NK Domzale ambapo tangu ametua nchini amekuwa gumzo kubwa kutokana na kuwavutia mashabiki.

Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram Dejan aliandika; "Nathibitisha mkataba wangu na waajiri wangu umevunjika, asanteni sana mashabiki kwa sapoti na mapenzi mliyonipa,"

Nyota huyo anaondoka kwenye kikosi hicho akiwa amefunga bao moja tu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar Agosti 20, wakati Simba iliposhinda mabao 2-0, mechi iliyopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hakuna lolote, mwandishi anaandika kisshabiki sana, eti simba magwiji wa mpira, upuuzi mtupu, timu haina kombe hata moja halafu mwandishi kichini chini anasifu

    ReplyDelete

Top Post Ad