Coastal Haitambui Uteuzi wa Mgunda Simba

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



KLABU ya Coastal Union imesema haina taarifa rasmi kutoka kwa Kocha Juma Mgunda wala mawasiliano yoyote rasmi na klabu ya Simba juu ya kijiunga kwake na Wekundi hao wa Msimbazi.

Uongozi wa Coastal umeeleza hayo katika taarifa iliyotolewa leo na Katibu wa timu, Omar Ayoub.

Septemba 7 Simba ilitangaza kumteua Mgunda kuwa Kocha wa muda wa klabu hiyo na tayari amesafiri na Simba kwenda Malawi ambako Septemba 10 itapamba na Nyasa Big Bullets katika michuano ya kufuzu Klabu Bingwa Afrika.

“Uongozi wa Coastal Union ulikuwa ukiendelea na mazungumzo na Kocha Juma Mgunda kwa ajili ya kuongeza muda wa kuifundisha timu yetu baada ya mkataba wake wa awali kuisha, hivyo suala la Kocha Juma mgunda na klabu ya Simba ni suala lake binafsi,” imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imesema katika kipindi hiki cha mpito Coastal Union itakuwa chini ya Mwalimu Kocha Joseph Lazaro.

Septemba 10 Coastal Union itaikaribisha Polisi Tanzania kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad