Walioshtakiwa kwa mauaji ya mtoto waachiwa huru

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Geita. Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza imewaachia huru washtakiwa wanne katika kesi ya mauaji ya mtoto Simon Kabula (2) baada ya upande wa Jamhuri kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Washtakiwa hao ni Ngeke Lunemhya, Mwajuma Petro, Ngeke Lunemhya na Maria Faida ambao wote ni ndugu.

Watuhumiwa hao walikuwa wakishtakiwa kumuua mjukuu wa mshtakiwa wa kwanza, Ngeke Lunemhya kwa kumdumbukiza katika shimbo la kuchimba dhahabu ili wapate dhahabu kwa madai kuwa waliambiwa na mganga.

Wakili wa Serikali, Bisela Alex ameileleza mahakama hilo leo Alhamisi Novemba 17, 2022 kuwa shauri hilo namba 78 ya mwaka 2020 Jamhuri dhidi ya Ngeke na wenzake watatu limekuja kusikilizwa lakini Jamhuri haina nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Kupitia kifungu cha 91 kifungu kidogo cha kwanza cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai Jamhuri imeomba kuondoa shauri hilo.

Kufuatia maombi ya wakili wa Serikali, Jaji Kamana Kamana amewaachia huru washtakiwa hao chini ya kifungu 191 cha Sheria ya Makosa ya Jinai namba 20.



-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad