Rais Samia "Nitaendelea Kuwanyofoa Huko"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema ameona mengi yakisemwa magazetini na mitandaoni kuhusu kitendo chake cha kuwanyofoa baadhi ya Wataalamu kwenye Sekta mbalimbali na kuwateua ambapo amesema haoni kama hilo ni tatizo kwakuwa wao ni Watanzania na wanastahili kufanya kazi sehemu yoyote ambapo amesisitiza kuwa ataendelea kuwateua ili wafanye kazi za kuijenga Nchi wakiwa ndani ya Serikali.



Akiongea Ikulu ya Chamwino Dodoma leo baada ya kuwaapisha Viongozi mbalimbali, Rais Samia amenukuliwa akisema “Kuna maswali mengi nimeyaona yakisemwasemwa kwenye magazeti kwenye mitandao, la kwanza ‘Mama ananyofoa Watu wenye akili huku anawachukua huku, huku sasa nani atafanya?’, hawa wote ni Watanzania na watafanya kazi popote na hakuna asiye na akili wote wana akili na kila Mtu akiwa anaonekana ana akili zaidi na Mimi namuhitaji zaidi”



“Kwahiyo tutaendelea kunyofoa huko na kuwaleta ndani waje watusaidie huku, sababu wakikaa nje kazi kulaumu Serikali bila kujua ugumu uliomo ndani ya Serikali, wakiingia tutafanya nao kwa pamoja twende”
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad