Fiston Mayele Na Clement Mzize Wagawana Ufalme Yanga Mashabiki Watamba

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


YANGA kwa sasa wanaringa kwa kuwa safu yao ya ushambuliaji inafunga mabao jambo ambalo ni furaha kwa benchi la ufundi la timu hiyo chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi, kutokana na wingi wa michezo na mashindano wanayoshiriki.


Yanga wanashiriki Ligi Kuu Bara, Kombe la Shirikisho la Azam Sports na Kombe la Shirikisho Afrika, jambo ambalo linahitaji mapumziko kwa wachezaji kwa kuwa michezo huwa ni mingi inafuatana mfululizo.


Jambo linalowapa jeuri ni kutokana na washambuliaji wake wawili, Fiston Mayele na Clement Mzize kugawana ufalme katika kupachika mabao ndani ya timu hiyo.


Mayele ndiye kinara wa upachikaji mabao katika ligi kuu akiwa anaongoza kwa kufunga mabao 15.


Katika kuonesha kuwa washambuliaji hao wamegawana ufalme wa kupachika mabao, Mayele akiwa ni kinara kwa upande wa ligi kuu, Clement Mzize naye amejiwekea ufalme wake.


Mshambuliaji huyo ndiye kinara wa upachikaji mabao katika michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports baada ya kufanikiwa kufunga mabao sita.


Mzize ana nafasi zaidi ya kufunga mabao baada ya Yanga kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo, huku Mayele naye akiwa na matumaini ya kuongeza mengine katika mechi saba za Ligi Kuu Bara zilizosalia.


STORI: MARCO MZUMBE

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad