Mama Kanumba Amtolea POVU Baya Mfalme Zumaradi "Nakupa Siku 7 Zumaridi Umlete Mwanangu"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Mama mzazi wa aliyekuwa msanii nguli wa Bongo Movies, Steven Charles Kanumba aitwaye Flora Mtegoha ‘Mama Kanumba’ amewaomba Watanzania wamsaidie kumshughulikia anayejiita Mflame Zumaridi baada ya kutangaza kuwa atamfufua marehemu Kanumba.


Zumaridi ambaye ametoka gerezani hivi karibuni baada ya kumaliza kifungo chake cha mwaka mmoja kwa makossa ya kusafifirsha watu kinyume cha sheria, amesema juzi Februari 26, 2023 kuwa atamfufua Kanumba na atamleta kanisani kwake Mwanza.


“Naomba Watanzania wenzangu msisaidie katika hili, kama wanawake wengine walioingia leba, nina uchungu sana, namshangaa huyu anayejiita mfalme Zumaridi, aliwahi kuniita kwake mwanza miaka kama saba imepita akidai kuwa Kanumba wanaongea naye, nikaenda sikuwahi kumuota wala kumuona pale Kanumba.


“Nashangaa jana anatangaza kwamba anamleta Kanumba, naomba Serikali na wanasheria wote mnisaidie, huyu mama anamtafuta nini mwanagu? Amuache apumzike kwa amanai. Kama anaweza kufufua akamfufue baba yake na ndugu zake.


“Kama anaweza kufufua akafufue kipenzi cha watu, Hayati Rais Magufuli, atamke wazi kama anaweza kumfufua. Mimi naumia sana ndugu zangu, miaka 12 mwanangu hayupo duniani. Yesu mwenyewe hajawahi kurudi kwa hiyo anamanisha alimchukua Kanumba kama msukule?


“Namuomba Rais Samia aingilie kati jambo hili, yeye anatafuta kiki lakini ananiumiza mimi. Huwezi kumfufua mwanangu Kanumba. Hata manabii na mitume hawajawahi kufufuka. Sasa ninakupa siku saba nimuone mwanangu Kanumba.


“Zumaridi aliwahi kuniita nikafika pale sikuwahi hata kumuota wala kumuona Kanumba, akaletwa dada kwamba ndiye huwa anaongea na Kanumba, nikasema basi huyo anapendwa na Kanumba mimi hanipendi.


“Hata waliponipeleka kwenye vyombo vyao vya habari nikiri kwamba nimemuona Kanumba nilikataa, nikasema siwezi kukufurahisha wewe Zumaridi nikamuudhi Mungu wangu.


“Tafuta kiki nyingine sio kwa mwanangu. Watu wananicheka miaka 12 mama Kanumba hachoki kulia, kilio kitaishaje kila siku yanaibuka haya? Kanumba aliambiwa ni Freemason nikakaa kimya. Huyu Zumaridi sitahangaika naye, namkabidhi kwa Mungu wangu aliye hai ashughulike naye,” amesema Mama Kanumba.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad