Maskini Justin Bieber Kuacha Muziki Kutokana na Afya yake Kuzidi Kuwa Mbaya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Kwenye ‘Agosti 13’ ya Fareed Kubanda (@therealfidq) kuna mstari maarufu unasema “U-superstar ni mzigo wa mwiba, ukiubeba unaumia” na ndicho kimemkuta Justin Bieber ambaye taarifa zinaripoti kwamba yupo mbioni kuachana na kazi ya Muziki.

Bieber anafikiria kuachana na kiwanda cha Muziki kwa ajili ya kujikita kwenye kuangalia afya yake pia na ndoa yake na Hailey. Taarifa zinaripoti kwamba JB amekuwa akitaabika na msukumo ambao unatokana na kubana kwa ratiba zake.

Kwa sasa Justin Bieber ameahirisha tarehe zote zilizokuwa zimebaki kwenye ziara yake (Justice World Tour) kufuatia kugundulika kuwa na ugonjwa wa Ramsay Hunt syndrome, ambao ulimfanya apooze kwa muda upande wa kulia wa uso wake.

Chanzo kimoja kimeuambia mtandao wa RadarOnline kwamba “Justin amekuwa hana furaha na mambo ya dunia kwa muda sasa, na mzigo wa umaarufu wake unamuelemea. Hata matabibu wake wamemwambia kwamba kama anachokifanya hakimpi furaha, anapaswa kufanya maamuzi magumu kukiweka pembeni.” Kilieleza chanzo hicho.

Watu wameenda ndani kabisa na kuchimbua kuwa ndio maana Justin Bieber mwezi January mwaka huu, alichukua maamuzi ya kuuza haki za Muziki wake (catalog) kwa $200M, takribani TSh. Bilioni 468 ikiwa ni miongoni mwa mipango ya kukaa mbali na masuala ya muziki.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad