Ticker

6/recent/ticker-posts

Mbunge Aliyepiga Sarakasi Bungeni, Apiga Tena Kwenye Mkutano

Nafasi za Ajira Serikalini Zilizotangazwa Wiki Hii Bonyeza HAPA

Nafasi za Internship Zilizotangazwa Bonyeza HAPA

Matokeo ya Form Four 2022 Bonyeza HAPAMbunge wa Mbulu Vijijini (CCM), Flatei Massay amepiga tena sarakasi mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo wakati wa mkutano wa hadhara wa kuhitimisha ziara ya Chongolo katika mkoa huo.


Massay amepiga sarakasi leo Machi 10, 2023 alipopewa nafasi ya kusalimia wananchi akiwa ni mmoja wa wabunge wa mkoa huo.


Akiwa mwenye furaha, Massay alisalimia wananchi "CCM Oyeee" na kuwauliza "nipige sarakasi?", wote wakaitikia kumruhusu apige.


Mbunge huyo akaweka kipaza sauti chini na kupiga sarakasi kwa kutembelea mikono mbele ya jukwaa kuu la viongozi wa kitaifa wa CCM akiwemo pia Waziri wa Maji, Jumaa Aweso.


Kitendo hicho kiliibua shangwe huku watu waliohudhuria mkutano huo wakiangua vicheko na kupiga makofi wakati mbunge huyo akitembelea mikono yake mbele ya jukwaa kuu.


Hii siyo mara ya kwanza kwa mbunge huyo kupiga sarakasi, alifanya hivyo pia bungeni Dodoma, Mei 2022 wakati wa mjadala wa hotuba ya bajeti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi akishinikiza kujengwa kwa barabara kuu katika jimbo lake.


Hata hivyo, Spika wa Bunge, alipiga marufuku sarakazi bungeni na vitendo vingine ambavyo haviruhusiwi kufanyika bungeni kwa mujibu wa kanuni za Bunge.

Post a Comment

0 Comments