Bado Pointi Tatu tu Yanga Bingwa Ligi Kuu Tanzania, Yatuma Salam South Africa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


BADO tatu tu Yanga bingwa! Ndivyo wanavyotamba mashabiki wa Yanga baada ya kushuhudia timu yao ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida Big Stars.

Katika mchezo huo ambao Yanga walicheza ugenini kwenye Uwanja wa Liti mkoani Singida, walitawala sehemu kubwa ya mchezo huo ambapo ndano ya dakika 10 tayari walikuwa wamekosa nafasi mbili za wazi kupitia kwa Clement Mzize na Kennedy Musonda.

Aziz Ki alifanikiwa kuipatia Yanga bao la kwanza la uongozi dakika ya 15 baada ya kupiga shuti kali kutoka nje ya eneo la 18 ambalo lilimshinda mlinda mlango wa Singida, Benedict Haule na kutinga wavuni.

Dakika ya 21 Mzize aliifungia Yanga bao la pili akitumia vyema asisti ya winga Mkongomani, Jesus Moloko ambaye alifikisha asisti ya tano msimu huu.

Singida Big Stars walijitahidi kurejea kwenye mchezo kwa kutaka kusawazisha makosa yao ambapo walifanya majaribio dakika za 20, 36 na 45, lakini kipa wa Yanga Djigui Diarra alikuwa imara kuokoa mikwaju hiyo ya Meddie Kagere na Bruno Gomes.

Kipindi cha pili kila timu iliendelea kutengeneza nafasi za kufunga, huku wakipokezana umiliki wa mpira kwa zamu.


Ushindi huo umeifanya Yanga kufikisha pointi 74 ambapo wanahitaji ushindi mmoja tu, katika michezo yao mitatu iliyosalia ili kutawazwa rasmi kuwa mabingwa wa Ligi Ku Bara 2022/23 kwani pointi hizo haziwezi kufikiwa na timu yoyote.

Ushindi huo pia ni ujumbe wa salamu kwa wapinzani wao wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Marumo Gallants watakaovaana nao Mei 10, mwaka huu.

Stori na Joel Thomas
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad