Huddah Kuwashtaki Wanaomtumia Kutapeli "Mtajua mimi ni mtoto wa gheto"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Huddah Monroe,
Huddah Monroe,


Mwanasosholaiti Alhuda Sonie Njoroge almaarufu Huddah Monroe, kwenye Instastory yake alidai kuwa ametosheka na habari ghushi zinazochapishwa kuhusu bidhaa zake.


Huddah aliwaonya Wanamitandao kuwa iwapo atawashtaki kwa habari ghushi kuhusu bidhaa zake basi watalazimika kulipa shilingi milioni 35 hata kama aliyechapisha ni maskini basi atalazimika kulipa yote anayopata kwa maisha yake yote


"Ukiwahi kusema bidhaa yetu ilikufanyia hiki na kile na ukijua kabisa ni uongo, tutakupeleka kwa daktari tutafanya vipimo vyote muhimu na kama ni uongo, utatulipa shilingi milioni 35 kwa tuhuma za uongo na kashfa," Huddah aliandika katika Instastory yake.


Huddah aliongezea na kusema kuwa kwa Miaka ijayo hachezi na brandi yake au jina lake kwani ilimchukua muda mrefu sana kufika hapo alipo.


"Mumenizoea sana na inatosha," mwanasosholaiti huyo aliyejawa na hasira aliandika.


Huddah aliwakashifu watu wanaomchukia akisema yeye si mtoto ambaye jina lake linaweza kuchafuliwa.


Katika chapisho lingine kali, Huddah alisema,"Nimejijengea jina kupitia jasho, bidii na uvumilivu wangu. Wewe umeingia media juzi unataka kung'ara na Huddah?


Yeyote atakayechapisha chochote kunihusu na ni uongo bila kutafuta ukweli, wewe na media house yako nitawashtaki hadi mtakapokuja na ukweli au kunilipa kwa miaka kumi na zaidi niliyofanya kazi hadi hapa nilipo. Siku za kutabasamu na kuziacha zipite zishapita. Ni wakati wa kunipigania hadi siku nitakayokufa."


Huddah alikiri kwamba kwa miaka kadhaa iliyopita aliwacha habari ghushi kumhusu zichapishwe. Ila kwa sasa hataruhusu kuharibiwa jina na wanaoandika habari ghushi kumhusu na kuhusu bidha zake.


"Mtajua mimi ni mtoto wa gheto. hamtanizoea kuanzia sasa hivi nimewanyamazia kwa muda mrefu siwezi kuruhusu mtu achapishe uongo kunihusu tena. Hao wa ficha kitambulisho changu, tutaona Hide Id yangu na utambulisho wako wa kweli mahakamani na mtanilipa mpaka mchoke wajinga."

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad