Jokate Mwegelo Afunguka Haya Baada ya Kumbeba Mtoto Mchanga Aliyeokotwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mkuu wa wilaya ya Korogwe, Jokate Mwegelo, ameeleza kuwa Wanawake wengi wakiwa wanatafuta watoto wapo ambao Mungu anawabariki kupata watoto lakini wanawatupa

Kupitia ukurasa wake wa #Instagram wa instagram ameandika………

“Huyu ni mtoto aliokotwa katika kijiji cha Kwenangu, Kata ya Mkumbara. Alitupwa na mama yake mzazi baada ya kuzaliwa majira ya saa 7 Usiku nakuoneka na wanakijiji majira ya saa 1 asubuhi Tarehe 16/5/2023 nakukimbizwa katika kituo cha Afya Mkumbara ambapo alipatiwa matibabu na baadae majira ya saa 11 jioni alihamishiwa Hospitali ya Wilaya ya Magunga katika Kitengocha kuwahudumia watoto NICU ambako aliendelea kupata matibabu na sasa Afya yake imeimarika na leo tarehe 23/5/23 anapelekwa kituo cha kulelea watoto yatima Ilente kilichopo wilayani Lushoto kwaajili ya malezi.

“Mtoto amepewa jina la Brigita Ustawi Korogwe, jina la DMO Korogwe Vijijini.

“Wakati Wanawake wengi wakiwa wanatafuta watoto wapo ambao Mungu anawabariki kupata watoto lakini wanawatupa. Niwasihi nafahamu kuna stress nyingi zinaambatana na kubeba mimba na hata malezi. Lakini baraka aliyotupa Mwenyezi Mungu ya kuleta kiumbe chake duniani kwangu Mimi naona ni thawabu na zawadi kubwa mno kuliko changamoto tunazopitia Kama wakina mama. Tukaze mwendo Mungu mwenyewe huleta baraka zake kupitia hawa Malaika na vizazi vyetu.

Nichukue fursa hii kuwapongeza madakatari wote na afisa ustawi wa jamii kwa kuokoa maisha Ya mtoto huyu wa kike ambaye naamini kwa ku-survive msukosuko huu Mungu ana sababu kubwa sana nayeye huku duniani.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad