Fahyma wa Rayvanny ajitapa kuwa na kwapa safi zaidi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

Fahyma wa Rayvanny ajitapa kuwa na kwapa safi zaidi

Mzazi mwenzake na msanii Rayvanny, Fahyvanny au ukipenda Fahyma kwa mara nyingine ameibua ‘challenge’ ya kuchekesha mtandaoni akijitapa na kujigamba kwamba hakuna mrembo anayeweza kumfikia katika watu wenye usafi wa kiwango cha juu kwenye kwapa.


Fahyma kupitia Instastory yake, alipakia picha akiwa ameonesha kwapa lake safi lisilo na hata chembe ya nywele na kutupa vijembe kwa wale ambao muda wote wanamchamba mchana na usiku.


Fahyvanny aliwapa ‘challenge’ wale wanaomchamba akisema kuwa kazi yao ni tantarira nyingi ila kwa usafi wa kwapa hawamfikii hata robo, na hata kufikia hatua ya kuwataka kupakia picha za makwapa yao ili kushindana kuhusu ni nani kati yake na wao mwenye kwapa safi.


“Mnaonichamba hebu mnyooshe mikono juu kwanza tuone kwapa,” Fahyvanny aliuliza.


Hata hivyo, baadhi walihisi kwamba mkwara huu uliuwa umemlenga Paula binti wa Kajala ambaye kwa muda wa siku za hivi karibuni wamekuwa wakichambana kwa vijembe vya nguoni kisa mwanaume wake, Rayvanny.


Paula alizidisha mashambulizi yake kwa Fahyma haswa baada ya mama huyo wa mtoto mmoja kumrudia Rayvanny kipindi ambacho msanii huyo aliachana na Paula ambaye awali aliingia kwenye moyo wake akijaribu kujinafasi kwenye kigoda kilichokuwa kimekaliwa na Fahyma.


Inaonekana ni kama Paula alishindwa kuziba pengo la Fahyma katika moyo wa Rayvanny na baada ya miaka kama miwili hivi ilimbidi msanii huyo wa Next Level Music kujirudi maosa yake na kumtafuta Fayma ambapo alimudhihirishia mapenzi ya kweli kwa kumshirikisha kwenye video ya ngoma yake ya Forever kama vixen wa Video.


Tangia hapo Paula hajatulia kabisa na michambo kwa wapenzi hao, hadi ikafikia kipindi kimoja Rayvanny akalazimika kumkanya Paula na mamake dhidi ya kutumia picha zake bila idhini yake katika kipindi cha uhalisia cha Behind the Gram.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad