Whozu afunguka uaminifu wake kwa Wema Sepetu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

Whozu afunguka uaminifu wake kwa Wema Sepetu

Mwanamuziki wa Bongo Oscar John Lelo almaarufu Whozu amekiri kwamba amezama kabisa kwenye dimbwi la mahaba na muigizaji Wema Sepetu.


Akizungumza na waandishi wa habari wa Tanzania, mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alibainisha kwamba mahusiano yake wa sasa yameundwa na mapenzi mazito ya pande zote mbili.


"Sasa hivi niko kwenye mapenzi mazito sana. Mwanamke niliye naye, Wema Sepetu ananipenda sana, na mimi ninampenda sana. Napendwa," Whozu alijigamba.


Aliongeza, "Nikifa leo, katika wasifu ambao mtasoma, msisahau kusema eti nilipenda sana."


Whozu aliweka wazi kwamba hajawahi kumsaliti Wema kimapenzi tangu walipojitosa katika mahusiano zaidi ya mwaka mmoja uliopita.


Alieleza kwamba mojawapo ya hofu zake kubwa maishani ni kumkosea muigizaji huyo na hivyo hawezi kupata ujasiri wa kumsaliti kimapenzi.


"Mwanamkewangu ni wa kwanza ninayeogopa kumkosea kwa chochote kile, ata kumhusu kwa kitu kidogo ninaogopa, sembuse kumcheat? siwezi! Nina mwaka sijacheat. Mimi sijui kucheat. Kucheat ya nini," Whozu alisema.


Wema na Whozu walijitosa kwenye mahusiano ya kimapenzi mwaka uliopita baada ya kuwa marafiki kwa muda mrefu.


Mapema mwaka huu, muigizaji huyo alifunguka jinsi alivyokutana na Whozu na hatimaye kuanza kuchumbiana mwaka jana.


"Tulikuwa Dodoma, nilikuwa nimeenda kwa ajili ya kazi. Yeye alikuwa amefika kwa ajili ya masuala yake mwenyewe," Wema Sepetu alisema wakati wa kikao cha Iftar nyumbani kwake mnamo mwezi Aprili mwaka huu.


Alisema baada ya kukutana mwaka wa 2019 walishiriki uhusiano wa kirafiki kabla ya kujitosa kwenye mahusiano mwaka jana.


"Tumekuwa marafiki. Wakati mwingine nilikuwa namshauri kwenye mambo yake ya mapenzi. Tulianza kuchumbiana mwezi wa nne mwaka jana," alisema


Mwimbaji Whozu alikuwa kwenye mahusiano mengine wakati alipokutana na muigizaji huyo na kuanza urafiki.


Sepetu hata hivyo ameeleza kuwa mahusiano ya awali ya mchumba huyo wake tayari yalikuwa yamefika kikomo walipoanza uchumba.


"Alikuwa na shida zake yeye na mtu wake. Mimi sikutaka kuingilia. Nilikuwa wa msaada kwa namna moja ama nyingine pale ambapo alihitaji sapoti. Tulikuwa naye kama rafiki kwa miaka miwili. Niseme nini, jambo moja lilipelekea jingine.. sijawahi kuvuruga mahusiano ya watu. Tukianza mahusiano alikuwa single sana. Alikuwa bila mchumba kwa takriban miezi mitano," alisema muigizaji huyo.


Wawili hao waliweka mahusiano yao wazi mwaka jana wakati mpenzi huyo wa zamani wa Diamond akiadhimisha siku ya kuzaliwa.


----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad