Mumewe Zari Hassan adaiwa kuwa mdogo sana na kukosa raha naye, alijibu vikali

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA






Siku ya Jumanne jioni, mwanasosholaiti Zari Hassan alichapisha picha zake kadhaa akijivinjari na mumewe Shakib Cham Lutaaya kwenye kilabu.

Zari alinukuu picha hizo akisema ni nyakati kama hizo ambapo huwa anajiachia na mpenzi huyo wa maisha yake.

"Wakati pekee utanishika nikiteleza... na mume wangu," aliandika chini ya picha hizo ambazo aliunganisha kuwa video.


Mamia ya wanamitandao walikusanyika chini ya chapisho hilo, baadhi wakitoa maoni mazuri huku wengine wakisema vibaya.

Baadhi ya wanamitandao walilalamika kuhusu tofauti kubwa kati ya umri wa Shakib na mama huyo wa watoto watano.

"Je, ni mimi tu ninayefikiria kuwa jamaa huyu ni mdogo sana?" beckleon.e alijibu chini ya chapisho hilo la Instagram.

Baadhi ya mashabiki waligundua sura ya huzuni ya Shakib na kudai alionekana kutoridhika na mwanasholaiti huyo wa Uganda.


"(Shakib) Anaonekana kukosa raha katika nyingi ya picha hizo," c_life_live alisema.

iam_makati alisema,"Ni kama Shakib aliwekwa kwenye picha."

Shabiki mmoja hata hivyo alibainisha kuwa kijana huyo Mganda ana umri wa zaidi ya miaka 30 na akadokeza kuwa dini ya Kiislamu, ambayo ni dini ya Zari na mumewe, inaruhusu mwanamke kuolewa na mwanaume mdogo kiumri.

Zari ambaye alionekana kuvutiwa na maoni ya shabiki huyo alijibu, “Waache wakabwe koo."


Zari Hassan na Shakib walifunga ndoa ya Kiislamu almaarufu Nikkah mwezi uliopita baada ya kuchumbiana kwa takribani mwaka mmoja.

Wawili hao walivishana pete katika hafla ya faraghani ambayo ilihudhuriwa na idadi ndogo ya watu wakiwemo wanafamilia na marafiki.

Katika picha na video hafla hiyo iliyofanyika chumbani ambazo zilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii, wapenzi hao walionekana wamevalia Kiislamu kabisa huku wote wakiwa wameketi kwenye mkeka uliotandikwa sakafuni.

Shakib alionekana akiinama kwa goti moja na kumvisha Zari pete ya ndoa kwa furaha kabla ya wawili hao kupigana mabusu huku watu wachache waliohudhuria hafla hiyo wakiwasherehekea kwa makofi.

Kwa sasa Zari ana umri wa miaka 42 ilhali mume wake Shakib alifikisha miaka 31 mwezi Disemba mwaka jana.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad