Mwamba Ajikata Uume, Kisha Kukimbilia Polisi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 30 Simon John, Mkazi wa Mtaa wa Msonobarini chini, Kata ya Msinjahili iliyopo Manispaa na Mkoa wa Lindi anadaiwa kujikata uume wake na kisha kukimbilia katika Kituo cha Polisi.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema Mwanaume huyo ambaye ni Mfanyabiashara alifika nyumbani kwake asubuhi majira ya saa 4 asubuhi akitokea kwenye shughuli zake na baada ya kuingia ndani kwake walimuona akitoka nje akiwa mtupu na anachuruzika damu sehemu za siri na kuelekea maeneo ya Baharini.

Majirani wamesema Mwanaume huyo alionekana Baharini akiwa ameshikilia pasi na akajitosa Baharini kwa lengo la kujisafisha na kukausha damu kabla ya kuamua kuelekea Kituo cha Polisi ambapo Polisi walimpeleka Hospitali ya Rufaa ya Sokoine kwa matibabu.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt Baraka Steven Mshango amekiri kumpokea Mwanaume huyo majira ya saa 4:30 asubuhi akiwa na majeraha katika sehemu zake za siri na uume wake ukiwa umeondolewa kabisa na kwa sasa amelazwa katika wodi ya uangalizi maalum.

Bado chanzo cha kujikata uume wake hakijajulikana
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad