Mwanamuziki Cheedy Aendelea Kumbomoa Harmonize

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

Mwanamuziki Cheedy Aendelea Kumbomoa Harmonize

Msanii wa Muziki wa kizazi kipya nchini, Cheedy amefunguka namna alivyotoka katika lebo ya King's Music akiamini ataenda kufanikiwa katika lebo ya Konde Gang lakini matokeo yake nako alienda kuangukia pua zaidi ya alikokuwa.


Cheedy amesema kuwa, wakiwa King's Music, yeye na Msanii mwenzake Killy walishauriana kuondoka kwenye lebo hiyo baada ya kuona hawakuwa na mkataba, lakini pia mipango yao ilikuwa inaenda taratibu tofauti na walivyokuwa wanataka.


Amesema wao walikuwa wanataka watoe nyombo back to back, lakini haikuwa hivyo, wakiwa King's Music walikuwa wanatoa nyimbo kwa kulegalega jambo ambalo lilikuwa linawanyima usingizini kwakuwa wao walitaka kufanya kazi zaidi.


Amesema baada ya kupeana nasaha na mwenzake Killy, walitoa taarifa kwenye uongozi wa Kampuni hiyo, na baada ya kuruhusiwa kuondoka wao wenyewe walimtafuta Harmonize kutaka awasaini kwenye lebo yake ya Konde Gang ambapo kwa kipindi hicho lebo hiyo ilikuwa ya moto na yenye ushindani mkubwa.


Baada ya kukubaliwa Harmonize aliwasaini haraka huku moja ya makubaliano yao yaliyoandikwa kwenye mkataba wao ni kutoa nyimbo tatu pekee kwa mwaka.


Zilipendwa huyo wa Konde Gang ameongeza kuwa, Konde Gang waliwasainisha mikataba kihuni-huni kwani baada ya kujiunga na familia ya Konde Gang walianza kuona mambo yakienda tofauti na walivyotarajia, ambapo hakukuwa na nyimbo tatu kwa mwaka wala moja.


Walijikuta wakiingia kwenye mtihani zaidi ya kule walikokuwa wametoka (King's Music) kwani wakiwa Konde Gang waliambulia nyimbo moja tu kwa mwaka nayo ilikuwa inaenda bila promotion huku Bosi wao akidiri kwenye mapenzi na mambo yake mengine zaidi kuliko kuwajali wasanii wake.


Baada ya mambo kwenda shagalabagala,ndipo wawili hao, Cheedy na mwenzake Killy waliamua kuondoka kwenda kutafuta maisha sehemu nyingine ili waweze kujipata, ambapo mpaka sasa bado wanaachia nyimbo kwa kusuasua wakiwa hawana menejimenti wanajisimamia wao wenyewe na kushikwa mikono na watu wao wa karibu.


Mpaka sasa wasanii hao hawana maelewano mazuri na mabosi wao ambao ni Alikiba na Harmonize na wamewablock kila sehemu.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad