Majibu ya Kusah baada ya Mose Iyobo kusema Kusah ni Kama Dada wa Kazi wa Aunty Ezekiel

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Majibu ya Kusah baada ya Mose Iyobo kusema Kusah ni Kama Dada wa Kazi wa Aunty Ezekiel

Staa wa Muziki wa Bongo Fleva na hiti meka wa wimbo pendwa wa (I wish), Kusah, amefunguka kuhusu maneno ya kejeli na dharau ambayo amekuwa akiambiwa na Moze Iyobo ambaye pia aliwahi kuwa kwenye mahusiano na Aunty Ezekiel ambapo walibahatika kupata mtoto mmoja wa kike kisha penzi lao liliishia kupasukiana vibaya na kujenga chuki kubwa.


Kwenye mahojiano mbalimbali na Wanahabari, Mose Iyobo amekuwa akisikika akimsema vibaya Kusah kuwa ni msanii ambaye hana pesa na analelewa na Aunty Ezekiel. Mose amedai kwamba ili Kusah aendelee kuishi na Aunty Ezekiel lazima amlee mtoto wake vizuri, ikiwa ni pamoja na kumuogesha, kumpeleka shule na kuhakikisha amekula vizuri, la sivyo penzi la wawili hao lingekuwa limekufa kama Kusah angekataa kutumika kama dada wa kazi.


Kwa upande wake Kusah amejibu madai hayo kwa kusema kwamba, kwanza hataki kumzungumzia Mose Iyobo kivyovyote vile, ilimradi yeye anajua anachokifanya, amesema yeye ni baba bora kwa mtoto wake na hata mtoto wa Mose anamlea kama mwanae, habagui na wala dharau za Moze hazimzuii kumpenda mtoto wake Cookie, amesema anapambana usiku na mchana kuhakikisha familia yake inakula vizuri na kulala pazuri hivyo anashangaa anaposikia maneno ya kwamba analelewa ikiwa kazi anazofanya zinaonekana.


Tangu aachane na Aunty Ezekiel, Moze Iyobo ambaye ni Mnenguaji wa Diamond Platnumz amekuwa akitapatapa kwenye mahusiano mbalimbali ambayo mengine yanadaiwa kuwa mahusiano bandia ambayo huwa anayafanya kwa lengo la kumuumuza Aunty Ezekiel na Kusah lakini amekuwa akitoka bilabila kutokana na penzi la Kusah na Aunty kuwa la kweli na lenye msimamo

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad