Waliofukiwa na Kifusi Kwa Siku 8 Waokolewa Geita, Walikuwa Wakitafuta Dhahabu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

Waliofukiwa na kifusi kwa siku 8 waokolewa

Wachimbaji wawili wa dhahabu Mpina Shukuru (29) mkazi wa Muganza Geita na Renatus Nyanga (35) Mkazi wa Sengerema wameokolewa wakiwa hai baada ya kukaa kwa muda wa siku 8 ndani ya shimo walilofukiwa na kifusi wakitafuta dhahabu katika mgodi wa Igalula uliopo wilayani Nyang’wale mkoani Geita


Wakizungumza na EATV katika eneo la tukio mashuhuda waliohusika kuwaokoa watu hao wanaipongeza serikali pamoja na uongozi wa mgodi huo  kwa jitihada walizozionesha mpaka kuwaokoa watu hao wakiwa hai.

 

Hussen Makubi Mwananyanzala ambaye ni Mmiliki wa leseni katika eneo hilo amesema eneo hilo la machimbo palipotokea ajali hiyo lilikuwa limezuiliwa kwa muda kutumika


"Walikuwa wanachimba eneo ambalo limezuiliwa kufanyia kazi na waliingia kinyemela, walikuwa watatu, wawili wakafukiwa mmoja akatoka akaja akatoa taarifa ofisini na sisi tukaenda tukaanza kuwaokoa tumetumia siku nane tukawa tumewaokoa na kwa sasa wako hospitali wanaendelea vizuri," amesema mmiliki huyo.


Princepius Mgishagwe ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya wilaya ya Nyang’wale amethibitisha kuwapokea majeruhi hao miili yao ikiwa imedhoofika sana kutokana na kutopata chakula kwa muda mrefu

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad