DODOMA: Wanaodaiwa kuwa wapenzi wakutwa wamefariki

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa




Dodoma. Watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni wapenzi wamekutwa wamefariki dunia huku mwanamke akiwa amechinjwa na mmwanaume ambaye hajafahamika jina akiwa na jeraha kubwa tumboni lililosababisha utumbo kutoka nje.

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia leo Jumatatu Septemba 18, 2023 katika Mtaa wa Oysterbay, Kata ya Dodoma Makulu kwenye chumba ambacho mwanamke aliyeuawa Samira Mathias alikuwa amepanga.

Akizungumza na Mwananchi katika eneo la tukio mwenye nyumba hiyo, Donald Nhembelo amesema alisikia kelele za kuomba msaada kutoka kwenye chumba cha mpangaji wake (Samira) saa 7.00 usiku.

Amesema baada ya kufika kwenye chumba hicho alisikia sauti ya mwanaume akiomba msaada ndipo alipouliza Samira yuko wapi na kujibiwa kuwa hawezi kuongea na yeye hawezi kusimama.


“Aliniomba nivunje mlango ili nimsaidie. Nilivunja ubao uliopo juu ya mlango (Venti) na kuingiza mkono kwa ndani na kufungua mlango na nilipowasha taa ndipo nilikuta Samira yuko juu ya kitanda amenyamaza,”amesema.

Amesema damu zilikuwa zimetapakaa kitandani na sakafuni huku mwanaume aliomba msaada ambaye hamfahamu akiwa amelala chini huku utumbo wake ukiwa nje.

Amesema baada ya kuona hali hiyo, aliripoti polisi ambao walifika kwenye eneo hilo ambao baadaye waliondoka na miili ya watu hao.


Balozi wa mtaa wa Oysterbay, Isaya Mabigiri amesema amepata taarifa za uwepo wa tukio kutoka kwa mwenye nyumba hiyo na alipokwenda alikuta miili ya watu.

_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad