Aliyekuwa mchezaji wa Fountain Gate Princess Academy Peris Oside raia wa Kenya amelalamika kupewa ujauzito na kiongozi wa klabu ya Fountain Gate Princess Academy wakati alipokuwa akiitumikia timu hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Klabu ya Fountain Gate Academy inasema klabu hiyo iliingia mkataba wa miaka miwili na mchezaji huyo na kisha mkataba huo ukavunjwa kwa makubaliano ya pande zote mbili na Peris akaondoka kikosini hapo.
Hivi karibuni klabu ya Fountain Gate Academy walipokea taarifa kuhusu swala hilo na kisha kumsimamisha kazi kiongozi aliyetajwa kuhusika ili kupisha uchunguzi licha ya yeye kupinga kuhusika.
Fountain Gate academy imelaani vikali matukio kama haya na kusisitiza kuwa klabu yao inaishi misingi ya soka la wanawake
Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA