Rais wa zamani wa Gabon Ali Bongo Odimba Aachiwa Huru, Afya Yatetereka

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Bonyeza Hapa

 

Rais wa zamani wa Gabon Ali Bongo Odimba Aachiwa Huru, Afya Yatetereka

Rais wa zamani wa Gabon, Ali Bongo Odimba aliyeondolewa madarakani katika mapinduzi ya kijeshi August 30,2023 ameachiwa huru.


@DWKiswahili_ imeripoti kuwa Rais wa mpito Jenerali Brice Nguema amesema Bongo yuko huru kuondoka Gabon na kusafiri kwenda Nchi za nje akitaka.


Akiisoma taarifa hiyo iliyosainiwa na Nguema, kanali Ulrich Manfoumbi Manfoumbi amesema kwa kuzingatia hali yake ya afya Ali Bongo Ondimba ana uhuru wa kutembea na anaweza kusafiri nje ya Nchi kama anataka ili kufanya vipimo vyake vya afya.


Bongo alipatwa na ugonjwa wa kiarusi October 2018 ambao ulimuacha na ulemavu wa mwili hasa matatizo ya kusogeza mguu wake wa kulia na mkono wa kulia.

_________

 Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo na Makampuni Bonyeza HAPA

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad