Yanga Kufanyiwa Kifuru Kuiua Al Merrikh Kwa Mkapa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





YANGA juzi ilikuwa uwanjani kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo lakini vichwani kwao wanajua kwamba wamebakiza dakika 90 tu kuchukua mzigo wa Sh100 milioni kutoka kwa matajiri wao.

Iko hivi. Yanga ilipomalizana na Namungo tu akili zao haraka zimeanza kuwapigia hesabu wapinzani wao Al Merrikh ya Sudan katika mchezo utakaoamua nani anakwenda makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga ndio iliyotanguliza mguu mmoja makundi baada ya ushindi mzuri wa mabao 2-0 ilioupata jijini Kigali, Rwanda ambako Wasudani ndiko walikochagua mechi zao za nyumbani zipigiwe huko.

Ushindi huo ni kama tayari mastaa wa Yanga wameshachukua nusu ya fedha, walizoahidiwa na matajiri wa klabu hiyo na kwamba wakiing’oa Merrikh watakabidhiwa fasta kiasi hicho cha Sh100 milioni.

Mbali na ahadi hiyo mastaa wa Yanga wanatambua kwamba bonasi hiyo itaongezeka zaidi katika mechi za hatua ya makundi ambapo kutakuwa na mgawanyo tofauti wa mechi za nyumbani na zile za ugenini watakazocheza.

Mmoja wa vigogo wa Yanga aliliambia Mwanaspoti kuwa, wameongeza dau kwenye hatua hiyo kwa lengo la kuhakikisha timu inafika mbali zaidi kwenye michuano hiyo ya CAF ambayo wana miaka 25 hawajawahi kutinga tena makundi tangu ilipofanya hiyo mwaka 1998 na kumaliza mkiani katika kundi walilopangwa.

Kigogo huyo (jina tunalo) alisema msimu uliopita wakati Yanga ikicheza Kombe la Shirikisho Afrika na kufika hadi fainali uongozi wa klabu hiyo ulifichua kwmaba kikosi chao kilitumia zaidi ya Sh1.5 bilioni kuwalipa bonasi pekee zilizochochea ushindi hadi ile ya mwisho ugenini dhidi ya USM Alger na kulikosa taji kwa faida ya bao la ugenini lililowabeba wenyeji baada ya matokeo ya mwisho kuwa sare ya 2-2. Katika mechi ya kwanza nyumbani Yanga ilifungwa mabao 2-1 na kushinda ugenini 1-0 kwa bao la penalti la Djuma Shaban aliyepo Azam sasa akisubiri kutambulishw
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad