Kenya: Mwanamke Aliyemchoma Daktari Visu Mara 25 Na Kumuua Anaswa Kwenye CCTV

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





Kurugenzi ya Upelelezi wa makosa ya jina nchini Kenya, DCI imeanzisha msako mkali na kutafuta taarifa za kusaidia kukamatwa kwa mshukiwa mwanamke wa mauaji ya Dr. Erick Maigo.

Tukio hilo limetokea Ijumaa ya September 15 asubuhi huko Woodley Annex – Upper Nairobi.


Dr. Erick Maigo ambaye ni mkurugenzi wa fedha wa hospitali ya Nairobi alikutwa akiwa amefariki dunia nyumbani kwake katika mazingira ya kutatanisha.

Wapelelezi wameendelea kufanya uchunguzi kujua ukweli wa tukio hilo la kinyama.

Upelelezi muhimu unaanzia kwenye video za usalama ambazo zimemnasa mshukiwa wa kike akiondoka kwenye nyumba ya Maigo. Mshukiwa huyo anaaminika kuhusika kwenye mauaji hayo kabla ya kukimbia kwa kutumia mlango wa nyuma.


Video za mwanamke huyo asiyejulikana ambaye kwa sasa ndio mshukiwa mkuu zimetolewa kwa umma.

Visu viwili vilivyokuwa vimejaa damu vinavyodaiwa kuhusika kwenye mauaji hayo vilikutwa kwenye eneo ambalo uhalifu umefanyika.

Wapelelezi wameutaka umma kutoa taarifa zitakazosaidia kunaswa kwa mshukiwa huyo.

Kwa mujibu wa ripoti ya uchunguzi, Erick Maigo alichomwa visu mara 25 na alifariki dunia kutokana kuvuja damu nyingi ndani na nje.

Uchunguzi huo ulifanyika wiki iliyopita baada ya mwili wake kupatikana nyumbani kwake Ijumaa iliyopita.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad