Yanga Yaingizwa Super League, Rais wa TFF, Wallace Karia Afunguka

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Yanga Yaingizwa Super League, Rais wa TFF, Wallace Karia Afunguka


Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Wallace Karia amesema mwakani 2024 kupitia mashindano ya African Football League (Super League) Yanga itakuwa moja wapo ya timu zitakazoshiriki kwani wanategemea kuwa na timu 24.


"Kwa mwaka huu tuna timu nane lakini makubaliano ni timu 24, ukanda wa CECAFA na COSAFA tunatakiwa kutoa timu nane mwakani hata Yanga itakuwepo,"


Karia pia amewapongeza maofisa habari wa timu zinazoshiriki michuano ya CAF ngazi ya klabu Ally Kamwe (Yanga), Ahmed Ally (Simba) na Hussein Massanza (Singida Fountain Gate) kwa kuungana kwa pamoja katika kufanya hamasa kuelekea katika michezo yao.


Aidha amezitaka klabu hizo kwenda kuwakilisha nchi vyema kwani katika mashindano ya kimataifa nchi ndio inashiriki.


"Naamini timu zetu zitafanikiwa kuingia makundi katika mashindano ya kimataifa na hayo ndio malengo yetu, Timu zinapocheza mashindano ya kimataifa tunaenda kama Tanzania tukirudi kwenye ligi yetu kila mtu apambane"

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad