Erling Braut Haaland Achoka Man City

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Erling Braut Haaland Achoka Man City

Erling Braut Haaland Achoka Man City

Mshambuliaji wa Kimataifa Manchester City, Erling Braut Haaland amekiri kuwa anapata tabu kukabiliana na ongezeko la kufuatiliwa kwa kiasi kikubwa ambalo amekuwa akipata katika miaka ya hivi karibuni.


Baada ya kuachana na Red Bull Salzburg ya Austria mwaka 2020, Haaland amefurahia kupanda kwa kiwango chake ambacho kilimfanya kukiwasha kwa kiwango kikubwa Bundesliga akiwa na Borussia Dortmund kabla ya kuvunja rekodi nyingi akiwa na Manchester City katika mechi za Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya.


Na sasa moja ya majina makubwa katika soka, Haaland amekuwa kivutio kikubwa baada ya Norway kuikanda Cyprus mabao 4-0 ukiwa mchezo wa kufuzu Kombe la Mataifa ya Ulaya (EURO2024) ambapo amefunga mawili na kufikisha jumla mabao 27 katika michezo 27 timu ya taifa.


Walinzi walilazimika kukimbilia uwanjani kumsaidia kukabiliana na kundi la mashabiki waliotaka kupiga picha naye na nafasi ya kuondoka na jezi yake katika mchezo huo.


"Ninaanza kuchoshwa kidogo na jina langu mwenyewe, lakini ndivyo ilivyo. Hakuna ninachoweza kufanya zaidi kuhusu hilo," Haaland amekiambia kituo cha televisheni cha TV2.


Katika ngazi ya klabu, kwa sasa Haaland ambaye ni raia Norway wa hajafunga bao katika michezo mitatu timu yake ilipokutana na Wolverhampton Wanderers, RB Leipzig na Arsenal.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad