Rais Samia "Nguvu ya Serikali yahamia Katesh Waliokumbwa na Mafuriko"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Rais Samia Kuhusu Mafuriko Katesh
Rais Samia Kuhusu Mafuriko Katesh

Rais wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ametoa salamu za pole kufuatia maafa yaliyotokea Kijiji cha Katesh Wilayani Hanang Mkoani Manyara leo na kusababisha vifo vya zaidi ya Watu 20 hadi sasa ambapo ametoa maelekezo kwamba nguvu zote za Serikali zielekezwe kwenye uokozi na kuzuia maafa zaidi kutokea.

Akiongea kutokea Dubai Rais Samia amesema “Kwa masikitiko makubwa tumepokea taarifa za kutokea kwa mvua kubwa Mkoa wa Manyara na kuleta madhara makubwa katika Kijiji cha Katesh, sisi tuliopo huku (Dubai) ambao tunashikiri mkutano wa mazingira tumesikitishwa sana na tukio hili lakini mipango ya Mungu ndivyo inavyokwenda tunatoa pole kwa Wahanga wa tukio hili”

“Nimeelekeza nguvu zote za Serikali zielekezwe huko kwenye uokozi na kuzuia maafa zaidi kutokea, Vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama nimevielekeza vifike huko, Wizara ya Afya kushughulikia majeruhi lakini pia Wizara ya Madini kuona nini kinatokea katika sehemu ambayo Milima imeonesha kutetemeka au kuporomoka”

“Nimemtaka Waziri pia anayeshughulika na maafa awepo huko, niwape pole Wananchi wote nami nipo njiani kurudi huko kuja kushirikiana na Wananchi katika hili lililotupata”
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad