Hafiz Konkoni aigomea Young Africans

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA






Juma moja likisalia kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa rasmi, huku Young Africans ikitajwa kushusha mshambuliaji mmoja kabla ya kufungwa kwa usajili, vita mpya imeibuka kutoka kwa mastaa wanaotajwa kuachwa huku Hafiz Konkoni na Gift Fred wakiwapasua vichwa mabosi wa klabu hiyo.

Young Africans inapambana kusaka saini ya Mshambuliaji atakayeiongeza nguvu eneo hilo akisaidiana na Kennedy Musonda, shida iliyopo ni namna Hafiz Konkoni anawapasua kichwa mabosi wa timu hiyo akiwataka wavunje benki ili awapishe wachezaji wengine.

Young Africans tayari imemsajili winga Augustine Okrah, lakini inasaka saini ya mchezaji mwingine wa eneo la ushambuliaji huku Konkoni aliyerejea mapema Dar kutoka Zanzibar ilipokuwa timu kabla ya kutolewa katikahatua ya Robo Fainali juzi Jumapili (Januari 07), imethibitishwa kuwa ameugomea uongozi kumtoa kwa mkopo kwenda timu yoyote, akitaka avunjiwe jumla mkataba.

Mbali na Konkoni pia taarifa kutoka ndani ya timu hiyo zimethibitisha kuwa mpango wa kuachwa kwa beki Gift Fred unaweza kuota mbawa kutokana na beki huyo kuonyesha uwezo mzuri kwenye michuano ya Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar.

Gift ndio lilikuwa chaguo la pili kupisha sajili mpya kwa mastaa wa kigeni ndani ya timu hiyo lakini kocha Gamondi ameonekana kuvutiwa na uwezo wa beki huyo kutoka nchini Uganda aliyetumika katika michuano ya Mapinduzi 2024 kutokana na safu ya ulinzi ya timu hiyo, hasa beki ya kati yote kuitwa timu ya taifa.

Ubora wa Gift anaouonyesha ndani ya timu hiyo nao unaongeza ugumu wa kufanya uamuzi kwa viongozi wa Young Africans hivyo kubaki wakiwaza wanamtoa nani na wanabaki nani ili kuingiza sajili mpya.

Chanzo cha kuaminika kutoka Young Africans kimeeleza kuwa, Konkoni aliondoka mapema baada ya kushindwana na viongozi kuhusiana na kuomba kupewa muda zaidi ili aonyeshe uwezo, huku viongozi wakimuomba wamtoe kwa mkopo katika moja ya timu zilizopo kwao Ghana.


“Ni suala la muda tu kwa mshambuliaji huyo kumalizana na klabu kwani mazungumzo yalikuwa ni kutolewa kwa mkopo, huku yeye mwenyewe akiomba kupewa muda wa kucheza ili aweze kuonyesha uwezo alionao” kimesema chanzo hicho na kuongeza,

“Mchezaji aligoma kutolewa kwa mkopo na kuuomba uongozi umalizane naye kwa kumlipa stahiki zake zote za mkataba ili aende kutafuta maisha mengine nje ya Young Africans kwa kutafuta timu anayoitaka yeye acheze.

“Kwa Gift pia mapya yameibuka anaonekana kumkosha Gamondi kwani amekuwa bora sana tofauti na alivyokuwa anachukuliwa mbele ya uwepo wa Dickson Job, Bakari Mwamnyeto ambaye pia mkataba wake unaelekea ukingoni na Ibrahim Abdallah ‘Bacca’ ambao wamejihakikishia nafasi kutokana na ubora wao, hivyo kumnyima nafasi ya kuonekana na sasa kabaki mwenyewe anafanya vitu vikubwa na kumpa wakati mgumu kocha kufanya uamuzi.”

Wakati hali ikianza kuwa nzuri kwa upande wa Gift, mtihani upo kwa Moloko na Skudu ambao wana kazi ya kufanya ili kujihakikishia nafasi ya kubaki.

Moloko mkataba wake unaisha mwishoni mwa msimu huu 2023/24, huku Skudu akiwa bado ana mkataba na timu hiyo.
 

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad