Makonda Amlipua Tundu Lisu 'Acha Kulia Lia, Acha Uoga'

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda amewataka CHADEMA kuacha kulialia kwenye vyombo vya habari kwa kudai wamenyimwa nafasi ya kufanya kipindi na badala yake kuwataka kwenda site kufanya mikutano ya hadhara na kuzungumza na Wananchi.

Mwenezi Makonda amesema CHADEMA wamekuwa watu wa kutengeneza namna ya kutaka kuonekana wanaonewa kisha kufanya malumbano tuu ilimradi wapate huruma ya wananchi na waonekane wao ni watu wa kuonewa ambapo amesema kufanya hivyo ni kuishiwa sera.

Pia, Makonda ameeleza kuwa CHADEMA walilalamika kutopewa uhuru wa kufanya mikutano ya hadhara lakini kwa upendo na dhamira ya dhati ya Rais Dkt. Samia kwa kuongoza Nchi kwa misingi ya kanuni yake ya 4R aliruhusu hilo, wakataka maandamano wakaruhusiwa, wakataka ruzuku wakapewa lakini bado kila kukicha wamekuwa watu wa kutengeneze mizingwe.

Mwenezi Makonda akizungumza kwenye mkutano wa hadhara Mbeya Mjini, amesema wazi bila kuficha kuwa CHADEMA wameonesha kushindwa kuwa na hoja na sera za kuwashawishi wananchi ndio maana wamekuwa wakimuogopa hata alipohitaji mjadala nao walimkwepa na tangu yeye ameanza ziara wao walisimamisha kabisa mikutano yao.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad