Mwili wa Mtanzania Aliyekuwa Akifanya Kazi Google Wapatikani Mtoni Baada ya Kupata Ajali ya Boti

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




MAREKANI: Mwili wa Mtanzania Abraham Mgowano aliyekuwa akiishi na kufanya kazi katika Kampuni ya Google kama Mhandisi wa Programu Endeshi (Software Engineer) umepatikana ukielea katika Mto Miami jijini Florida baada ya kuanguka toka kwenye Boti (Yacht)

Abraham aliripotiwa kupata ajali Februari 24, 2024 akiwa na wenzake 12 pamoja na Kapteni wa Boti hiyo. Polisi walianza kumtafuta kwa kutumia Boti nyingine na Helikopta bila mafanikio hadi walipopata taarifa za kupatikana kwa mwili huo ukielea Februari 27, 2024

Kwa mujibu wa taarifa, Abraham alikuwa Mfanyakazi wa Google kwa miaka 9 baada ya kuwa mmoja wa Wanafunzi bora kutoka Chuo Kikuu cha Stanford. Baadaye aliajiriwa kama Mshauri wa Masuala ya Kompyuta chuoni hapo kwa mwaka mmoja

Aidha, Mtanzania huyo alikuwa kati ya Wanafunzi Bora 12 waliofaulu vizuri Mtihani wa Kidato cha 4 mwaka 2007 ambapo walipata nafasi ya kukutana na kupongezwa na Rais Jakaya Kikwete

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad