Diamond Platnumz Ampa Rick Ross Maua yake Kwa Kussuport Mziki wa Africa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



@DiamondPlatnumz jana amefanya live ‘convo’ ya Instagram na Staa wa Hiphop kutoka Miami, Marekani Rick Ross @RichForever na kuzungumza mengi ikiwemo kumpa maua yake kwa jinsi alivyoanza kuupa support muziki wa Afrika kitambo hicho hata kabla ya Wasanii wengine wa Marekani hawajaanza kuuzingatia.

Platnumz amemwambia Rick Ross kwamba anampa heshima kubwa sana kwa kitendo chake cha kuushika mkono muziki wa Afrika miaka mingi iliyopita wakati huo alipoanza kwa kufanya kolabo na P Square wa Nigeria.

Kwa upande mwingine, Diamond hakusita kumpa Rapper huyo maua yake mengine kwa jinsi alivyokuwa Mtu poa ‘humble’ wakati waki-shoot video ya wimbo wa ‘waka’ miaka sita iliyopita ambapo Director wa video alikosea kumpa Diamond muda sahihi wa kutakiwa kufika location na badala yake Rick Ross akawahi kufika bila Diamond kuwepo, kitendo ambacho Diamond alidhani angemkuta Ross kakasirika kwa sababu amechelewa lakini ikawa tofauti na akamwambia asihofu.

Kolabo ya Diamond Platnumz ft. Rick Ross ambayo video yake ilifanyika Marekani, iliachiwa December 8 2017 ambapo mpaka sasa ina zaidi ya views milioni kumi na nne laki tisa na comments zaidi ya elfu saba mia tano YouTube.

Nyoosha kidole juu kama unatamani Wakali hawa waingie tena studio !!!
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad