Paul Makonda Awashukia Baadhi ya Viongozj wa CCM Wanaojaribu Kumtofautisha Rais Samia na Magufuli

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Paul Makonda Awashukia Baadhi ya Viongozj wa CCM Wanaojaribu Kumtofautisha Rais Samia na Magufuli

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda, amewataka viongozi wa chama hicho na watu wanaojaribu kumtenganisha Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na Hayati Dk. John Magufuli, waache mara moja. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza katika hafla ya kupokea ndege mpya ya Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL), leo Jumatatu jijini Dar es Salaam, Makonda amedai kuna viongozi uchwara ambao wanajipendekeza kwa Rais Samia ili kumfanya kama sio sehemu ya Magufuli.

“Kuna kasumba ya ujinga unaoendelea wa kutaka kumtofautisha Dk. Samia na Dk. Magufuli, huwezi kuwatenganisha hao watu na viongozi wengi wanafiki wanaotafuta kujipendekeza kwa Dk. Samia, kila wakipata jukwaa wanataka kumfanya kama Dk. Samia si sehemu ya Dk. Magufuli. Kama msemaji wa chama tukazunguka na ilani ya chama chetu anachokifanya Dk. Samia ndicho ambacho alikifanya Dk. Magufuli,” amesema Makonda.

Makonda amesema “na walisimama wakazunguka katika taifa hili wakatafuta kura kwa pamoja, huwezi ukawatenganisha na waziri mkuu wao yule pale, Kassim Majaliwa, ningetamani leo iwe ndiyo siku ya mwisho ya unafiki wa viongozi na wanasiasa uchwara wanaopambana kuwatenganisha viongozi hawa.”


Makonda alitoa kauli hiyo akizungumzia mafanikio ya miaka mitatu ya Rais Samia madarakani, aliyepewa mamlaka Machi 19, 2021 baada ya Magufuli kufariki dunia akiwa madarakani. Tangu alivyoingia madarakani Rais Samia amekuwa akiendeleza miradi iliyoachwa na mtangulizi wake, ikiwemo ununuzi wa ndege kwa ajili ya kuimarisha ATCL.

“Mafanikio haya tunayesherehekea wote kwa sababu chama ni kimoja, serikali ni ya CCM na nyie wananchi mliipigia kura,” amesema Makonda.

Kauli ya Mikonda imekuja siku kadhaa tangu Rais Samia kuweka bayana kwamba yeye hana makundi na kwamba yeye anafanya kazi na makundi yote. Alitoa kauli hiyo wakati akitaja sababu za kufanya mabadiliko ya wakuu wa mikoa na wilaya, aliyoyafanya hivi karibuni.

“Mwanzo niliwaambia mlitarajia nitawateua kwa makundi, lakini mimi Samia sina kundi, mkijitazama hum ohayo makundi mnayojua makundi yenu nyote mpo humo ndani, ninachotaka mimi watanzania kwa pamoja tufanye kazi tusogeze nchi yetu mbele, sina kundi sasa wale wanaosema huyu ni wa mama huyu sio wa mama, mimi mama nina watoto wote,” alisema Rais Samia.

Mwanahalisi
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad