Rais Samia Atengua Uteuzi Wa Viongozi Watatu, Ateua Wengine

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Rais Samia Ametengua uteuzi wa viongozi watatu. Waliotenguliwa ni Prof Jamal Katundu aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji ambaye nafasi yake imechukuliwa na Mhandisi Mwajuma Waziri.

Mwingine aliyetenguliwa ni Damas Mfugale aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii (TTB) ambaye nafasi yake imechukuliwa na Ephraim Mafuru.

Pia Rais Samia ametengua uteuzi wa Richard Kiiza aliyekuwa Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Uhifadhi Eneo la Ngorongoro (NCAA).

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus imeeleza kuwa, pia Rais Samia amemteua Ally Gugu kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ambapo kabla ya uteuzi huo, alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma.

Pia amemteua Kaspar Mmuya kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma ambapo kabla ya uteuzi, alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad