Ray Kigosi nini Shida? Gazeti lahoji Kupungua Mwili Kwake.

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Wiki kadhaa zilizopita paparazi wetu alishtuka alipomuona Ray kwenye ‘bethidei’ ya mwigizaji sistaduu Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ ndani ya Hoteli ya Shamoll iliyopo Sinza ya Lion, Dar akiwa amekongoroka na kuibua maswali kwa wahudhuriaji.
Ray Kigosi Mwaka Huu
Akiwa ukumbini hapo, minong’ono ilienea kuwa Ray alionekana kukondeana katika kipindi kifupi huku baadhi ya watu wakisikika wakiulizana kulikoni kwani alikuwa meza moja na bonge la mtu, Jacob Steven ‘JB’ hivyo kumfanya kuonekana mdogo mno.


VIWANJA VYA LEADERS
Akiwa kwenye Viwanja vya Leaders, Kinondoni, Dar wiki iliyopita, Ray aliibua mshtuko kwa mara nyingine hadi jamaa mmoja anayedhaniwa kutokuwa vizuri kichwani kumfuata na kumuwakia akimuuliza kwa hasira kuwa kulikoni akondeana kiasi hicho.

UZINDUZI WA WEMA
Kwa mara nyingine, Ray alizua hofu alipohudhuria kwenye uzinduzi wa ofisi ya Wema Sepetu uliofanyika maeneo ya Kinondoni, Dar ambapo alipoingia watu walipigwa butwaa wakimtazama na wengine kumuonea huruma wakidhani anaumwa.
Ray Kigosi Mwaka Jana

IJUMAA WIKIENDA LATAKA MAJIBU
Kwa nyakati tofauti, wanahabari wetu walizungumza na Ray ambaye alitoa majibu ya kukinzana na kuzidi kutia shaka.
Ray alimwambia mmoja wa waandishi wetu kuwa kilichosababisha akongoroke kiasi hicho ni mazoezi makali anayofanya ili kupunguza unene.
Katika majibu mengine kwa mwandishi wetu mwingine, Ray alidai kuwa anafanya ‘dayati’ ikielezwa kuwa ikishafika saa 11:00 jioni ndiyo mwisho wake wa kula msosi lengo likiwa ni kupunguza mwili uliokuwa umefumuka.
Kama mtu alimuona Ray kwenye Matamasha ya Serengeti Fiesta mwishoni mwa mwaka jana, akikutana naye lazima amtazame mara mbilimbili hivyo Ijumaa Wikienda lipo mzigoni kutafuta undani wa madai kuwa huenda staa huyo mkubwa anaumwa kufuatia majibu tofauti aliyoyatoa.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tatizo wabongo ukipungua tu unaumwa,unene c afya kwanza unene ndo ugonjwa.eti mtu akinenepa ndo mafanikio tubadilike tusilee miili tufanye mazoezi!!

    ReplyDelete
  2. na ndo maana mtanzania akifikisha miaka 50 kwisha kabisa na anaonekana ni kizee haswaaa.kuwa na tumbo au mwili mkubwa sio afya ni magonjwa sugu yanakunyemelea.

    ReplyDelete

Top Post Ad