Wema na Diamond Washindana_Pesa Inaongea

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


WAKATI Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu akionesha jeuri ya fedha kwa kufungua bonge la ofisi ya kuzalisha filamu, zilipendwa wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amemjibu kwa kukamilisha mjengo wa maana uliogharimu Sh. milioni 260 hivyo kwa pamoja kuthibisha msemo kuwa fedha inaongea, Ijumaa Wikienda lina data kamili.


Katika uzinduzi huo ambao Ijumaa Wikienda lilialikwa, Wema ndiye alikuwa wa kwanza kumshtua mama yake mzazi, Mariam Sepetu na mastaa mbalimbali (akiwamo Diamond), Jumatano iliyopita na kuzindua ofisi yake inayojulikana kwa jina la Endless Fame Films iliyopo Mwananyamala- Komakoma, jijini Dar.



ILIKUWA ‘SAPRAIZI’
Pamoja na mkali huyo ambaye ni sura ya mauzo kwenye gemu la filamu za Kibongo kumualika mama yake, ilibainika kuwa hakuwa amemtaarifu kabla kuhusu umiliki wa ofisi hiyo hivyo ilikuwa ‘sapraizi’ kwa mzazi huyo.
“Mama hii ndiyo ofisi yangu ambayo maandalizi yake yalianza tangu Juni, mwaka jana na sikutaka kukwambia hadi ilipokamilika ili iwe sapraizi,”  Wema alimwambia mama yake mbele ya wageni waalikwa na kuongeza:
“Nia na madhumuni ya ofisi hii ni kukuza vipaji vya wasanii wachanga hivyo nakaribisha chipukizi wa filamu waje kujiunga kwenye kampuni yangu.”
Bila kutaja gharama za ofisi hiyo, Wema alisema kwa kifupi kuwa imemgharimu mamilioni ya shilingi huku akiainisha vitu vilivyosheheni ndani kama jiko, ofisi yake, sehemu ya kunywea kahawa, kupumzikia wageni, vyumba viwili vya wahariri wa video pamoja na choo cha ndani.


MASTAA WALIOHUDHURIA
Siku hiyo ilipambwa na mastaa mbalimbali wa filamu kwa ajili ya kumpa sapoti mwenzao (Wema) ambaye ameonesha kupiga hatua kubwa kwenye sanaa wakiongozwa na Vincent Kigosi ‘Ray’, Jacob Steven ‘JB’, Single Mtambalike ’Richie’, Issa Mussa ‘Cloud’, Hartman Mbilinyi na Husna Posh ‘Dotnata’.

DIAMOND ALIKUWA WAPI?
Wakati mastaa waliofika kwenye sherehe hiyo ya Wema wakijiuliza juu ya kutohudhuria kwa Diamond, taarifa zilizonaswa na gazeti hili zilidai kuwa alikuwa katika mishemishe za kumjibu Wema kwa kuzindua mjengo wake wa kisasa uliopo Tegeta, jijini Dar.



TUJIUNGE NAYE
Akizungumza na paparazi wetu akiwa kwenye eneo ilipo nyumba hiyo ambayo ilikuwa ikifanyiwa ‘finishing’, Diamond alisema kuwa nyumba hiyo yenye thamani ya Sh. milioni 260 ni zawadi kwa mama yake Sanura Kassim ‘Sandra’.
“Mama yangu ndiyo kila kitu kwangu, mara ya kwanza nilimnunulia gari aina ya Toyota Alteeza nikaona haitoshi, nikaamua kumjengea hii nyumba ambayo itakuwa kama urithi wake hata nikifa leo,” alisema Diamond.



NI BONGE LA MJENGO!
Diamond alimzungusha paparazi wetu na kujionea mjengo huo wenye vyumba vinne vya kulala ambavyo vyote ni ‘self contained’ (chumba chenye choo na bafu), studio kubwa ya kurekodi muziki, eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya kujenga bwawa la kuogelea ‘swimming pool’, uwanja wa basketball na sehemu maalum ya kufanyia mazoezi (gym) ambapo alisema hadi ifikapo Septemba, mwaka huu kila kitu kitakuwa kimekamilika.

BONGE LA KIWANJA
Ukiachana na ukubwa wa nyumba hiyo, uwanja ambao ameuzungushia uzio wa ukuta kuna nyumba nyingine ndogondogo tatu ambazo kwa mujibu wa staa huyo wa Songi la Kesho, zitakuwa zikipangishwa.





----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sijaelewa ni nyumba yake.... Or yamama yake?km ya mamayake chumba kwaajil ya gym! Mazoez,swimming pull!studio yakurekod 4wat kwa mamayake????

    ReplyDelete
  2. Daaah hawa bongo flava na movie mwisho watatuambia hata saa ngapi wameenda kunya, kutiana , kujamba na kadhalika.
    Sina wivu na maendeleo ya mtu ila kujenga, kununua gari au kufungua ofc nayo ni issue kweli? Ina maana mahekalu, magari na ofc wameanza wao? Wafanye tu kimya kimya watu watasoma no mpya wenyewe bana.

    ReplyDelete
  3. Mwisho wawo ni ni hasa wanataka...diamond acha kujipimanishana na mwanamke.kesho atakupa kitu mwake mwake na utamupa yote hayo bila kujikubuka kua unaitaji na ww k2

    ReplyDelete
  4. mmh na wewe blogger nani kakwambia ni 260.m acha kuweka habari zisizo za maana,and yeye ndio wa kwanza kunga?? acheni ushamba

    ReplyDelete

Top Post Ad