Rose Ndauka Asema "Mchoro wa Tattoo Aliyo Chora Mchumba Wangu ni Dhahiri Ananipenda"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



MSANII wa filamu nchini Rose Ndauka afunguka juu ya tatoo  alizochora mchumba wake Mariki Bandawe, zinazoonyesha mchoro wa kopa . Alisema kupitia mchoro huo ni dhahiri kuwa mchumba wake amedhihirisha kuwa na mapenzi ya dhati

Rose alilazimika kufunguka juu ya hilo baada ya kupokea maswali mengi kutoka kwa baadhi ya mashabiki wake kwenye mtandao wa kijamii 'Facebook' baada ya kuituma picha hiyo inayomuonyesha mchumba wake akiwa na mchoro kwenye bega lake la kushoto

Akizungumza na jarida la Maisha Rose alisema kuwa mchoro wa mchumba wake ni dhahiri kuwa ana mapenzi ya dhati kwani ni wanaume wachache wanaweza kufanya kitendo alichokifanya yeye na kutuma picha kama hiyo ambayo inaonekana na watu wengi


"Unajua mpaka mtu inafikia hatua ya kuweka wazi ni kwamba unajiamini na chaguo lako na pia kwa upande wangu inaonyesha kunijali na kunilinda na baadhi ya magonjwa maambukizi kwa kutojihusisha na mwanamke mwingine," alisem Rose

Pamoja na hayo alizungumzia juu ya harusi yake ambayo amesema kuwa muda ukifika ataweka wazi tarehe na mwezi wa siku yao ya kufunga ndoa

Picha hiyo ilionekana kuleta utata baada ya mchumba wake kuituma picha kwenye mitandao ya kijamii 'facebook' huku baadhi ya mashabiki wakituma maoni yao juu ya picha hiyo na kutaka kufahamu nini maana ya alama iliyokuwepo kwenye picha
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. It might actually do easy effect jailbreaks from old iPhones and
    iPods. Some websites like Youtube.com do not present this method.



    my web page Installous iOS 7 (intra.phimart.com)

    ReplyDelete

Top Post Ad