Kinana kupitia Wanasheria amuandikia Msigwa kumtaka amuombe radhi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Omar Kinana, kupitia kwa wanasheria wa LAW OFFICES OF ERIC S. NG'MARYO wa Moshi amemuandikia Mbunge wa Iringa Ndugu Peter Msigwa agizo la kumtaka amuombe radhi kwa matamshi ambayo kinana anadai ni ya uongo kwamba,

"Nakuandikia kwa maagizo niliyopewa na mteja wangu, Ndugu Abdulrahman Kinana, kufuatia matamshi yako ya uwongo ambayo yamemkashifu, kumfedhehesha na kumshushia hadhi, Matamshi hayo uliyoyatoa mchana wa tarehe 21 April, 2013 katika mkutano wa hadhara wa kisiasa uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mbugani, Wilaya ya Nyamagana, jijini Mwanza. Mkutano huo ulihudhuriwa na watu wengi. Pamoja na watu hao walikuwepo pia waandishi wa habari, wakiwepo wanahabari wa magazeti, radio televisioni. Habari zenye Maneno yako ya Kashfa zimeenea nchi nzima na duniani kote kwa njia ya habari elektoniki, ikiwepo mitandao ya kijamii. Habari hizo zinaendelea kusomwa hadi sasa, na zitabaki kuwa kumbukumbu ya kudumu katika intaneti na kwenye hifadhi nyingine za habari" hiyo Para ya kwanza,

Para ya Pili ina hit point sasa, kwamba "Katika Mkutano huo, ulisikika ukisema maneno mengi ya Kashfa kwa mteja wangu, yakiwemo haya yafuatayo: Kinana (na naomba waandishi w habari mnisikie na nyie usalama wa Taifa mkapeleke habari) hana sifa za kupita barabarani na kuwaambia watanzania waiamini ccm. Kinana mikono yake si misafi hata kwenye NASACO, Shirika la Meli Tanzania, kuna harufu ya ufisadi ndani yake, ajibu hapa... Kinana Meli zake ndio zinahusika kubeba mapembe nchi hii, hajajibu hoja hizo! kwa siku katika nchi hii tembo sitini na saba wanauwawa...

Hao ndio wanaokifadhili Chama cha Mapinduzi wakina Kinana halafu wanakuja eti kuwashawishi watanzania muwasikilize na kwamba Chama cha Mapinduzi eti ni kizuri. Halafu leo tukikaa ndani ya Bunge tunapojaribu kuwatetea wananchi tumeacha majimbo yetu, Haya mambo ninayaongea ni hatari kwa sababu haya yote ni majangiri ni organized crime ni mtandao wa kimataifa uko duniani kote. unaweza ukatuua lakini wabunge tumesimama tunawatetea.."

Hivyo anamtaka Msigwa amuombe msamaha yaishe au la atamvuruta mahakamani, tena kwa vitisho katika para ya mwisho anasema "Nakuangaliza na kukutahadharisha kwamba iwapo hutatimiza matakwa ya Mteja wangu kama yalivyoainishwa kwenye barua hii, basi kesi itakayokuja dhidi yako itakuwa na madai makubwa na mengi kuliko yale yaliyotajwa humu, na unaweza kubebeshwa mzigo wa uharibifu, hasara na madhara uliyomsababishia Mteja wangu, pamoja na gharama za kesi nzima, ambazo zote zinaweza kufikia mamilioni ya Shilingi za Kitanzania"

Kuna para kumi na mbili, nimeweka attachment, na inapatikana ukurasa wa ishirini na tano wa gazeti la mwananchi, sina hakika juu ya magazeti mengine.

Sina hakika kama kazi ndio imeanza au imefikia Mwisho.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad