AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA
Raja Casablanca imepiga hodi Msimbazi kutaka kumsajili Kiemba baada ya kuvutiwa naye wakati walipomwona akiichezea Timu ya Taifa (Taifa Stars) dhidi ya Morocco zaidi ya wiki moja iliyopita.
Akizungumza na Mwanannchi jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Simba Zakaria Hanspope alisema, kiwango hicho cha fedha ndiyo thamani ya sasa ya Kiemba.
“Tayari tumezungumza na Raja Casablanca na kweli wameonyesha nia ya kumtaka Kiemba, lakini kwetu hakuna namna yoyote ya kumtoa bila Sh500 milioni kuwekwa mezani,” alisema Hanspope.
“Nilipokwenda kwao (Morocco) Rais wa klabu alikuwa Uturuki, tunasubiri arejee ili tuwatumie mchanganuo mzima wa mauzo ya Kiemba,” alisema.
Hanspope, alisema angependa kuona klabu yake inafanya biashara ya kuwauza wachezaji kwa faida. Tunatakiwa kuwalipa makocha, kuingia mikataba na wachezaji, mambo yote haya yanahitaji pesa. Hatuwezi tena kufanya biashara isiyo na faida kwa upande wetu,” alisema zaidi bosi huyo.
NAFASI ZA AJIRA
JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA
GOODLUCK
Halafu kazi halisi ya wanaojiita wadhamini wa Simba ni ipi?au ni usajili wa mbwembwe 2 na kufukuza makocha?
ReplyDelete