MAJAMBAZI WAVAMIA BENK JIJINI DAR ES SALAAM NA KUPORA ZAIDI YA MILIONI 150

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Majambazi saba akiwemo mmoja ambaye amevalia sare za polisi wameiteka benki ya I&M  jijini Dar es Salaam na kuchukuwa fedha zinazohisiwa  kuwa  ni zaidi ya shilingi milioni 150 na kutokemea kusikojulikana.

Tukio hilo limetokea katika benki hiyo iliyoopo katika makutano ya mtaa wa Indira Gandi na Mosque ambapo baadhi ya mashuhuda wameelezea tukio hilo lilivyokuwa.
  

Akizungumza katika eneo la tukio kamanda wa polisi mkoa wa Ilala kamanda Marieta Minagi amesema bado wanaendelea kufanya uchunguzi wa tukio lenyewe ingawa  mpaka sasa ni kama milioni zaidi  150 zinahisiwa kuibiwa.
  

Naye mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meki Sadiki akiwa katika eneo hilo amesema  matukio ya Kuiba fedha katika benki yanazidi kushamiri na hivyo kuna haja ya taasisi husika kujipanga  upya.
  
Hata hivyo ITV ilishuhudia baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo wakipandishwa katika gari la polisi lenye namba za usajili  T220 AMV na kuondoka  nao kwa ajili ya mahojiano  zaidi.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hao wafanyakaz wa hiyo Bank watakuwa wanajua kinachoendelea.Alafu pia inashangaza,huyo jambazi aliyevalia sare za police kazitoa wapi kama si police wenyewe kujihusisha na uhalifu?

    ReplyDelete
  2. Halafu mnakaribisha wawekezaji, kuna nchi huwezi hata siku moja ukasikia mlio wa risasi.hata watalii hawawezi kuja huko, hakuna amani

    ReplyDelete

Top Post Ad