MWANAMKE AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA MITANO JELA BAADA YA KUMTUPA MTOTO WAKE CHOONI

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwanamke mmoja mkazi wa Manga A Jijini Mbeya amehukumiwa kifungo cha miaka 5 jela kwa kosa la kutupa mtoto wake chooni. Mwaka huu katika eneo hilo baada ya watoto waliokuwa wakicheza kugundua kuwepo kwa Mtoto katika choo cha shimo. 

Mtuhumiwa baada ya kukamatwa amekiri kutenda kosa hilo na kwamba alifanya hivyo baada ya mzazi mwenzie kumkataa.

Ameongeza kuwa amelazimika kutupa katika choo cha jirani kwa sababu ni cha shimo tofauti na chao ambacho asingeweza kutupa mtoto huyo.

Rukia Haruna (31)  akitolewa nje  na Askari wa Jeshi la Polisi akitolewa nje ya  Mahakama kwenda Gerezani kutumikia kifungo cha miaka 5 Jela  

Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Archiles Mulisa mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, Zabibu Mpangula, amemtaja Mtuhumiwa kuwa ni Rukia Haruna (31) mkazi wa Manga A Jijini Mbeya na kwamba kosa lake ni kinyume cha kifungu  218 kifungu kidogo cha 35 sura ya 16 ya mwaka 2002.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

15 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ungefunga maisha .mtoto hana kosa yeye mzazi aloamua kumleta duniani

    ReplyDelete
  2. Wee wee toka zako wangemfunga maisha afu iweje

    ReplyDelete
  3. mbona mmemuhurumia ilikuwa mumpige kifungo cha maisha aona raha yake.

    ReplyDelete
  4. Mtoto anamleta yeye dunian,af anamwua et atashindwa kumlea, mbona mnatudanganya?mashiz wanazaa na wanalea hawaui watoto afu wewe na akil zako timamu unamwua unasingizia kushindwa kulea wakt una mambo yako binafs,achen hizo bahnaaa,jifunzen kujitegemea wanawake,huyo unaemwua ndo angekusaidia badae

    ReplyDelete
  5. huyo mama wa kufungwa miaka mitano?huyo alitakiwa aozee jela.mshenzi mkubwa huyo,na nn hasa kilichomfanya afanye hivyo,mpumbavu xana huyo dada.

    ReplyDelete
  6. sheria zirekebishwe hapo ilitakiwa baba alomkana mtoto afunge na mama pia wa mtotopia afungwe

    ReplyDelete
  7. mh sasa huyo siameua hiyo si nikesi ya mauaji kwanini afungwemiaka 5a wakati tuliambiwa sheria inasema ukiua unafungwa maisha hapo hamkumtendea mtoto haki

    ReplyDelete
  8. mwanaume alikotaa mimba ndo afungwe maisha mbwa uyo alivyokuwa anamwaga sperms zake bila kondomu ye alijiona mgumba,wanatuonea sana wanawake baadh ya wanaume ni mbwa koko 2!

    ReplyDelete
  9. huyo mama afungwe maisha au anyongwe afu baba naye afungwe miaka mia akafie gerezani

    ReplyDelete
  10. Afungwe alieua,wafungwe wote kwan mwanaume kaua? Nyie vip bahna

    ReplyDelete
  11. Janamke roho katili, lingefungwa maisha, na kuliko kumtupa chooni c bora hata ungeenda kutelekeza kwenye get ya kanisa au hosptl, lione kwanza. Blk beauty A town

    ReplyDelete
  12. angetupwa nayeye kwenye kwenye choo ya ,mahakama ausikie muziki

    ReplyDelete
  13. Ukatili uliopitiliza wanawake wana roho ngumu sana

    ReplyDelete
  14. Si bora angewapa wanawake wanaotafuta watoto na wapo wengi? jamani huyo mwanamke amwogopi MUNGU? angetupwa yeye angekuwepo? kwanini akatili maishia ya hicho kichanga? kwani ajui roho uwekwa na MUNGU? amemkosea sana MUNGU na pia sisi wote na amemkosea sana huyo mtoto anyongwe nae afe kama huyo mtoto, naumia sana sababu na mimi ni mjamzito natarajia kupata mtoto na ninajua ujauzito ulivyo na shida mpaka unampata mtoto kwanini abebe alafu atupe? angemlaza ata barabarani jamani wakina mama tutamwona MUNGU? tusali, tuombe ili shetani asituzingire tuombee familia zetu na watoto wetu tunaopewa na MUNGU.

    ReplyDelete
  15. Jamani msimlaumu huyu mwanamke huenda kichaa cha mimba alikipata baada ya kujifungua but also mwanaume hapa atakuwa kachangia lazima labda alimkataa mtoto hii inatia hasira sana mimi hii ya mwanaume kunikataa wakati napata mimba imenitokea na nikawa natamani sana kutoa hata mimba ili nisilete mtoto apate shida ulimwenguni lakini namshukuru mwenyezi mungu na mama yangu mzazi akawa mstari wa mbele kunishauri na kuwa na mimi karibu mwisho wa siku nikachukulia poa tu na wala nikawa siwazi tena nikajifungua salama mtoto ..hapo ndo niliposhikwa na hasira mpaka nikatamani kuua mwanangu tukose wote mwanaume wangu aliyenitia mimba na kuikataa akawa anamtaka mtoto nusu nilikuwa kama chizi ilibidi mama anihamishe mkoa na nikaenda sehemu ambayo mwanaume huyo hajui niliko hadi leo na mtoto wangu anaendelea kukua vizuri ili akili ilinituma hata kuua mtoto jamani cha msingi wanaume myaangalie haya mtoto ni malaika usimkatae kabla hajazaliwa na akizaliwa umuone binadamu na kumtaka awe wako inauma sana sio siri...........

    ReplyDelete

Top Post Ad