PICHA NA TAARIFA KAMILI JINSI DADA WA MH:FREEMAN MBOWE ALIVYOKUTWA NA MAUTI NA WALIONUSURIKA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Na Mashaka Mhando,Korogwe

DADA wa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amefariki papo hapo baada ya gari alilokuwa akiendesha kupasuka tairi ya mbele na kuingia chini ya daraja baada ya kupinduka na kusababisha watu wawili kufa na wengine watatu kujeruhiwa vibaya.
Dada huyo, Grace Aikaeli Mbowe,  anayesadikiwa kuwa na umri kati ya miaka 47 hadi 50, alikuwa akiendesha gari yenye namba T 277 CAJ aina ya Toyota Cresta akiwa na mumewe  aliyefahamika kwa jina la Ibrahim Lukindo (52), wakitokea Jijini Tanga, walipata ajali hiyo eneo la Kabuku wilayani Handeni.
Kamanda wa polisi mkoani Tanga (ACP) Costatine Massawe alisema kupitia Ofisa wake wa upelelezi mkoani Tanga, Bw Aziz Kimata, kwamba

 ajali hiyo ilitokea majira ya saa 1:30 asubuhi jana katika eneo hilo baada ya gari hilo kupasuka tairi ya mbele kulia na kisha kuingia chini ya daraja lililokuwepo eneo hilo.

"Ni kweli kuna ajali ilitokea eneo la Kabuku gari aina ya Cresta lililokuwa likiendeshwa na ndugu inavyosemekana wa Bw Freeman Mbowe, limepata ajali baada ya kupasuka tairi la mbele na kuacha barabara na kuingia chini ya daraja dereva anayeitwa Grace Aikael Mbowe na mtu anayesemekana ni mumewe anayeitwa Ibrahim Lukindo, wamefariki na watu watatu waliowachukua wamejeruhiwa," alisema RCO Kimata.

Aliwataja waliojeruhiwa kuwa ni pamoja na Bw Ridhiwani Bakari (29) aliyekuwa na mkewe Zeddy Nzuke (29) raia wa Kenya aliyekuwa na mtoto wake mwenye umri wa miaka miwili na miezi minne aliyefahamika kwa jina la Mariam Ridhiwan ambao kwa sasa wamelazwa katika hospitali ya Magunga wilayani Korogwe.
RCO Kimata aliyezungumza kwa niaba ya kamanda huyo wa polisi alisema chanzo cha ajali hiyo inasemekana kimetokana na kupasuka kwa mpira huo na mwendo kasi wa kawaida na kwamba majeruhi na maiti zi9mehifadhiwa kwenye hospitali hiyo.
Mwandishi wa habari hizi, aliyefika kwenye hospitali hiyo na kuzungumza na Ridhiwani pamja na mkewe ambaye amelazwa wodi namba mbili ya wanawake katika hospitali hiyo, alisema kwamba ndoto zake za kufanya kazi Dar es salaam zimezimika ghafla kutokana na kwamba alikuwa aende kupamba kazi ya uofisa ugavi katika taasisi moja ya fedha ya marehemu Mbowe Jijini Dar es salaam.
"Nilikuwa naenda kupewa kazi na mama Mbowe katika Institution yake ya Micro-Financial Jijini Dar es salaam, mimi ni procurement (Mgavi-manunuzi) na ni Mkenya kwetu ni Eastern Province Kang'undo na nimeolewa na bwana Mtizedi...Lakini sasa ndoto zangu za kufanya kazi Dar es salaam zimezimika ghafla," alisema Zeddy akiwa kitandani amelala na mwanwe ambaye alikuwa haongei tangu amefika katika hospitalini hapo.
Mumewe na mwanamke huyo akizungumzia ajali hiyo alisema kuwa hakuwa akijua kwani alikuwa amelala dakika tatu kabla ya kutokea ajali hiyo ambapo alishtukia yeye, mkewe na mwanawe wametupwa chini kwenye majani wakiwa hawajijui na walikimbizwa katika hospitali hiyo ya Korogwe.
Ridhin ambaye ni mkazi wa Nguvumali Jijini Tanga, alisema safari yao hiyo ilikuwa ifanyike Jumamosi mchana lakini kutokana na na kuchelewa kwa wenyeji wao hao, waliondoka Tanga kwenye hoteli ya Doliphin walikolala majira ya saa 11:00 alifajiri kwa ajili ya kwenda Jijini Dar es salaam.
Muuguzi wa zamu wa hospitali hiyo Bi Nayela Missingo alikiri kuwapokea wagonjwa hao ambapo alisema wanafanya jitihada za kuwahamishia katika hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es salaam mtoto Mariam ambaye amepata majeraha katika kichwa chake na kwamba tangu afikishe hospilaini hapo hakuwa katika hali nzuri, haongei walakunyonya.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Pole sana ndugu yetu.

    ReplyDelete
  2. Pole sana kamanda Mbowe,Mungu akupe subira katika kipindi hiki.kigumu.

    ReplyDelete
  3. Pole kamanda mbowe,Mungu awatie nguvu kipindi hiki cha majonzi

    ReplyDelete
  4. pole saca muheshimiwa mbowe,mungu akutie nguvu

    ReplyDelete
  5. Poleni sana na Mungu awasimamie ktk kipindi hiki kigumu

    ReplyDelete
  6. Mungu wa hekima awape faraja kipindi chote cha majonzi kamanda wetu watz tunaukubali mchango wenu.

    ReplyDelete

Top Post Ad