SEREKALI YA KENYA YAISHANGAA MAREKANI KWA KUSHAURI RAIA WAKE WASIENDE KENYA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Baada ya magaidi kuvamia kituo cha biashara cha Westgate nchini Kenya wiki iliyopita  ,Marekani imetoa onyo kwa raia wake kuacha kusafiri kuelekea nchini humo.

Kitendo hicho kilipokelewa kwa hisia tofauti na Serikali ya Kenya kwa kudai kwamba hatua hiyo iliyochukuliwa na Marekani  sio sahihi.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya ililaani vikali hatua ya Marekani ya kuwaonya raia wake kufanya safari nchini Kenya.

Taarifa hiyo iliitaja hatua hiyo kuwa, haina umuhimu na pia ilitolewa katika wakati ambao sio mwafaka.

Ripoti hiyo iliongeza kuwa, shambulizi la Westgate jijini Nairobi, ni tatizo la ulimwengu mzima hasa kwa kuzingatia kuwa, hata Marekani yenyewe imekwishaathiriwa na vitendo kama hivyo vya kigaidi.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hawana lolote hao wamarekani wao wanyewe ndio magaidi wakubwa, marekani ni taifa linalochukiwa na watu wengi duniani, gorge bush ameua maelfu ya watu huko asia lakini hakupelekwa the haege ni viongozi tu kama luto ndy wanapelekwa huko. Poleni ndugu zetu wakenya obama sio mkenya hata kama baba yake alikuwa mjaluo. Jitumeni kutafuta mtafanikiwa tu.

    ReplyDelete
  2. kwani alquda hawafiki huko american waja ujinga obama kifo ni kokote

    ReplyDelete
  3. hii kweli kali hadi wazee wa kuleta F.B.I wanagwaya.
    waafrika tubadilike tuache kupelekeshwa na matakwa ya hawa watu wa magharibi.

    ReplyDelete
  4. MAMBO YA NGOSO MWACHIE MWENYEWE NGOSO,, MMAREKANI KATAHADHARISHA TU WATU WAKE WAO WAKENYA WANA BIFU LAO NA OBAMA,, NDIO MAANA WANAFIKIRIA VIBAYA,, WATAYAMALIZA WENYEWE INSHALLAH!!!!

    ReplyDelete
  5. Watanzania nendeni kenya

    ReplyDelete
  6. Wakenya wamelikoroga sasa watalinywa wenyewe.
    Majwshi yao yatoke Somalia ndio watapona
    Marekani wameshajitoa wakati mwanzo walikuwa wanawapa moyo wakenya waende kupigana.

    ReplyDelete
  7. Alianza Obama akafuatia bush ,Oprah Clinton na family yake wali switch trip ghafla no Kenya mhhhh some thing is serious wrong

    ReplyDelete
  8. Am proud being Tanzanian,though this people( kenyans) wanatudharau sana....

    ReplyDelete

Top Post Ad