UJENZI WA BARABARA ZA JUU (FLYOVERS) KUANZA 2014

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MRADI wa Ujenzi wa barabara za juu unaotekelezwa na Serikali ya Japan, unatarajiwa kuanza mwanzoni mwa 2014. Hayo yalibainika jana baada ya Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli kufanya majadiliano na Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada na kukubaliana kuanza mchakato wa ujenzi wa barabara za juu na upanuzi wa barabara eneo la Bendera Tatu hadi Kamata. Katika majadiliano hayo, Balozi Okada alimhakikishia Dk. Magufuli kwamba miradi yote inayofadhiliwa na Japan itaanza kutekelezwa rasmi mwanzoni mwa 2014.

Balozi Okada alisema kuwa hivi sasa Japan kupitia kampuni zake za ujenzi, imejipanga kukamilisha miradi yote kwa mujibu wa makubaliano. “Januari 2014 tutaanza na upanuzi wa barabara inayoanzia eneo la Bendera Tatu hadi Kamata, wakati upanuzi huo ukitekelezwa, mchakato wa ujenzi wa barabara za juu unaendelea.

“Kwanza hivi sasa tumeanza mchakato wa kuwapata wakandarasi ambao ni makini kutoka Japan, ambao watatekeleza miradi yote kwa wakati uliopangwa hususani barabara za juu katika eneo la TAZARA na maeneo mengine.

“Hii ni miradi mikubwa sana na inahitaji umakini mkubwa ili kulinda heshima yetu kati ya Tanzania na Japan, katika historia yetu hatujawahi kuharibu kazi kutokana na umakini wetu,” alisema. Kwa upande wake Dk. Magufuli alimhakikishia balozi huyo kwamba taratibu za kusafisha maeneo ya miradi zinaendelea kufanyika na baadhi ya maeneo zimekamilika.

Dk. Magufuli alisema sehemu ya barabara ya kuanzia Bendera Tatu hadi Kamata eneo la Gerezani, limekuwa likisababisha msongamano mkubwa kwa watumiaji wa barabara ya Kilwa kutokana na barabara hiyo kuwa nyembamba.

Alisema kukamilika kwa barabara hiyo kutakuwa ni faraja kubwa kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, ikiwa ni pamoja na watumiaji wanaelekea mikoa ya Kusini mwa Tanzania. Dk. Magufuli alisema mradi wa barabara kuanzia Mwenge hadi Tegeta unaendelea vizuri na kusisitiza mradi huo upo katika hatua za mwisho kukamilika.

“Tunataka kupunguza msongamano wa magari hapa Dar es Salaam, pale Mwenge yamebaki madaraja mawili ambayo yanashughulikiwa, pia zipo sehemu ambazo zilionekana kuwa na kasoro nazo zinarekebishwa. MWISHO

Tarime, Rorya kupata umeme Desemba (pg 2) Na Doroth Chagula, Mara KAZI ya kupeleka umeme katika vijiji 11 wilayani Tarime na Rorya, mkoani Mara, inatarajia kukamilika, Desemba mwaka huu. Kazi hiyo inayotekelezwa na Kampuni ya kizalendo ya Namis Corporate Ltd, inatarajiwa kugharimu, Sh bilioni 7.2.

Mhandisi wa kampuni inayotekeleza mradi huo, Haidu Ruta, alisema utekelezaji wa mradi huo uko katika hatua za mwisho na kubainisha maeneo yatakayonufaika ni pamoja na Hospitali ya Masongo iliyopo wilayani Rorya.

Ruta alivitaja vijiji vya Nyachabakenye, Marasibora na Nyarombo kuwa ni miongoni mwa maeneo yatakayofikiwa, huku wateja 124 wa awali wanatarajiwa kupelekewa huduma ya umeme katika maeneo hayo. Vijiji vingine vitakavyonufaika na mradi huo unaosimamiwa na Wakala wa Umeme Vijijini (REA), ni pamoja na Kungombe, Kabasa, Salama kati, Mcharo, Sizaki, Chanjunge, Kichumbwa na Shule ya Sekondari Unyari.

Wateja 308 wa awali nao wanatarajiwa kufikiwa na huduma ya umeme, huku wateja 74 katika eneo la Itiryo nao watafikiwa na huduma hiyo. Meneja msaidizi wa ufundi wa REA, Boniface Gissima, alisema awamu ya pili ya utekelezaji wa miradi hiyo ya umeme inayohusisha wilaya zote za Mkoa wa Mara utagharimu zaidi ya Sh Bilioni 48 na kupeleka umeme katika vijiji 204, huku wateja 14,600, wanatarajiwa kufikiwa na huduma hiyo ifikapo 2015.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mange mango mange mango

    ReplyDelete
  2. serikali ilichelewa mno kufanya haya mambo

    ReplyDelete
  3. Ifike wakati Serikali yetu sasa iache ubabaishaji. kwani mipango inaonekana kuwa ni mizuri sana kwa Taifa. Lakini jee utakelezawaji ni kwa % ngapi? Hilo ndio swali.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Fanya yako kaka naona pcha imewakera,,,jiachie jiachie kwa raha zako

      Delete
  4. Afu wew apo juu nani kacma anataka kukuona sura ysko embu jieshimu fala we

    ReplyDelete
    Replies
    1. hadi jina kaweka,nadhani anasubiri kupewa zawadi kama mtoa maoni mzuri

      Delete
  5. Nanyi c' muweke za kwenu kwn kunaubaya gn? Wapumbavu wakubwa

    ReplyDelete
  6. Acheni kumsakama kila m2 na maamuz yake,,,kuma mama zenu.mbwa nyie aweke pcha aweke pumbu si lake nyie inawahusu nini,,,mbwa kweli,,,makafiri kama nyie nikunyonga,,,2 hampaswi kuwepo ktk ulimwengu kama huu,,,

    ReplyDelete
    Replies
    1. Watu kama nyie shida yenu kubwa ni kukosa shule, mtu aliyeelimika hatukani ovyo

      Delete
    2. we fala jifunze kuwaheshimu wanawake, hicho kiungo unachokitukana kimekuleta duniani

      Delete
  7. bo chog mutoto muziri sana wewe, mimi iko ona picha yako kwenye comment...omba namba yako, mimi penda wewe, mimi iko itwa Iddi Omar.. je facebook iko wewe??

    ReplyDelete

Top Post Ad