WEMA SEPETU: AANIKA HISTORIA YA MAISHA YAKE ISOME HAPA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wema Sepetu alizaliwa tarehe 28 September hivyo leo ni birthday yake. Taja wasichana wote wa Bongo Movies wanaotamba Tanzania, usipoliweka jina la Wema Sepetu orodha haijakamilika. Wema Sepetu ni supastaa asiyefutika kwenye vichwa vya habari vya magazeti ya udaku na websites/blogs. Mfahamu zaidi kwa undani leo anaposherehekea siku yake ya kuzaliwa katika mahojiano haya aliyoyafanya na Bongo5 kwaajili ya jarida la Mzuka.
_DSC1063 copy
Kwenu mko wangapi na wewe ndio mtoto wa mwisho?
Kwetu sisi tuko wanne na mimi ndio mtoto wa mwisho, nina dada watatu. Wa kwanza na wa tatu wako Marekani, wa pili yupo hapa hapa, ameolewa ana familia yake. Wa kwanza yuko kule anafanya kazi ana mtoto mmoja. Wa tatu yuko kule anasoma na anafanya kazi 
Miaka mitano kabla ya mwaka 2006, Wema alikuwa ni msichana wa aina gani?
Wema alikuwa ni msichana wa kawaida. Wakati ule ulikuwa ukiniuliza unataka kuwa nani ukikua ningekujibu nataka kuwa air hostess sababu dreams zangu zilikuwa ni kuwa air hostess, sijawahi kufikiria kabisa kuingia kwenye fame. Though nilikuwa nawaangalia watu kama Ray C, K-Lynn, Kwasababu mimi nilikuwa nasoma academic na shuleni kwetu nakumbuka tulikuwa tukitoka ile home time kulikuwa na duka fulani hivi la mpemba tunaenda tunakula sambusa nini, so magari yatapita nini and we would see Ray C and everybody will go like ‘you see Ray C’ you know, kwahiyo we go crazy over superstars na watu famous. 
Kiukweli I never so myself kuwa katika this position ambayo niko. Kwahiyo nilikuwa tu msichana ambaye sina ndoto za kuwa star lakini nilikuwa tu nawashangaa masupastaa. My dad amekuwa anapenda sana mashindano ya Miss Tanzania and kila mwaka alikuwa anamake sure kwamba amenunua tiketi ya kwenda kuangalia Miss Tanzania. 
So nakumbuka ilikuwa ni mwaka wa akina Sylvia Bahame tumekaa nyumbani amekosa tiketi. Akakaa akasema ‘kumbe ukiwa umekaa nyumbani ndio unaenjoy vizuri kuliko hata kwenda pale’ akasema ‘one day nawish one of my beauties hata kama hatoshinda, nikilipia tiketi naenda nikijua kabisa nimeenda kumlipia binti yangu.
So sikukiweka kichwani hicho kitu lakini after kuingia katika whatever na nini, so siku nimekaa na dad nikamwambia ‘dad unakumbuka kuna siku ulisema hivi’ akasema ‘yes I remember’ . Hata Mange Kimambi alivyokuja kuniapproach, alivyoniona Sleep Way akaniambia kwamba anataka niingie katika mashindano, nikamwambia kwamba mimi nina wazazi wangu, siwezi nikaamua tu mimi mwenyewe na mimi nakaa na wazazi, so nilivyoongea na mama akasema ‘ongea na baba yako’ nikampigia simu baba alikuwa kipindi hicho Dodoma, akaniambia ‘fanya my beauty nitakusupport’, hakuthink twice alinipa go ahead kabisa.
Kabla ya Miss Tanzania, ni watu wachache sana waliokuwa wakimfahamu Wema Sepetu, ni vipi Miss Tanzania ilibadilisha maisha yako hasa kutokana na watu kuanza kufuatilia maisha yako na chochote unachofanya?
Ni kitu ambacho nilikipata bado nina umri mdogo and nilikuwa sijajiandaa, nilikuwa naichukulia tu poa this whole issue ya kuwa kwenye spotlight. Nilikuwa sidhani kama itakuwa vile kwasababu kama wanavyosema experience ni bora uexperience mwenyewe usione kwa wenzako so nilivyokuwa naichukulia ni tofauti na ilivyokuja kuwa kwasababu mimi nilikuwa naichukulia tu ‘kuwa star raha’ umeenda watu wamekushangaa nini lakini nilivyokuwa nimeingia sana katika ile spotlight nikasema kumbe ooh my God it’s this hard.
Kwahiyo ikawa ni kitu kilichonipa wakati mgumu sana kukizoea like mpaka sasa hivi naweza kusema kwamba ile umetoka kila mtu kakuangalia nini, it’s not an easy task, yaani haizoeleki hiyo hali yaani kila siku unazidi kuiona mpya kwasababu there is no place unaweza ukaenda ukawa na privacy yako, yaani upende usipende lazima utakuwa ni attention kwa watu, lazima watu watakuangalia. Sometimes natamani tu na mimi niwe Wema lakini huwezi sababu all eyes on you. And a lot of times as a normal human being kuna time unahisi you just be yourself lakini inakuwa ni time chache chache sana. The only place where I can be myself is in my room and in my house, out of my gate you cannot be yourself.
Kuna wakati wowote uliwahi kujuta maisha ya ustaa baada ya kuwa Miss Tanzania?
Yes, nimewahi kujuta lakini mwisho wa siku huwaga nasema kwamba mwenyezi Mungu ndio anapanga kwasababu kama mwenyezi Mungu ndio amenipangia hivi nisingefika hapa kwanza, kwahiyo regrets zinatokea kwa kila mtu, lakini siwezi kusema kwamba zimetoka kwa mara nyingi, labda mara moja mara mbili na zinatokea pale tatizo linapotokea, hauwezi ukapata regrets kama hakuna tatizo.
Ukiwa staa kila mtu atataka awe rafiki yako, na kabla ya kuwa Miss Tanzania ni wazi ulikuwa na marafiki uliokuwa ukihang out nao hapa na pale, uliendelea kuwa na urafiki nao, ama baada ya kuingia maisha hayo ikakuwia vigumu kuwa nao tena pamoja?
Nina marafiki mpaka sasa ninahangout nao wanakuja mpaka nyumbani lakini hatushei sana zile common interests kama zamani because once upon a time tulikuwa tuko wote on the same rank. So nilivyokuwa nipo kwenye spotlight obvious nimekutana na watu wengine wapya watu ambao naonana nao katika kazi zangu za kila siku, because apart from being Miss Tanzania, I am also an actress, kwahiyo nakutana na wasanii wengine ambao labda nakaa nao kwa muda mrefu sana kwahiyo utajikuta tu unashare nao common interests sababu unafanya nao kazi pamoja. 
Ulikuwa na boyfriend tayari? 
Yes nilikuwa naye
Kuna wakati wowote aliwahi kujihisi inferior kutokana wewe kuwa maarufu? Ulifanyaje kumweka sawa?
Well, si unajua zile za kishuleshule, zile za kitoto naweza kusema. Sana sana ukishafika ile o-level nini utakuwa na yule boyfriend ambaye unaamka tu asubuhi umeshavaa unasema sasa hivi naenda kuonana na boyfriend wangu, ukisharudi kutoka shuleni from there nyumbani, no boyfriend. Yeah nilikuwa naye, in the beginning alivyojua kwamba nashiriki Miss Dar Indian Ocean akaniambia kwamba ‘ukishiriki mimi nisahau, sitaweza kuwa na wewe tena’, nikamwambia, why? Akaniambia ‘utakuwa upo kwenye public’ nikamwambia ‘okay fine’, nikamdanganya kwamba sishiriki. 
So siku moja gazeti la Mwananchi pale katikati kulikuwa na picha yangu kubwa ‘Miss Dar Indian Ocean kushindana kesho’ and lile gazeti kuanzia naingia shuleni naingia kila mtu ananiambia ameniona kwenye gazeti. So kitu cha kwanza nikafikiria ‘Mungu wangu yule mtu akiliona’ so sikuonana naye the whole day.
Nikiwa nyumbani ndio nikamuona anakuja kalishikilia, nikawa namsikiliza. Akaniambia, ‘nimeona gazeti lako and ndio hivyo kwahiyo umeshanidhihirishia kwamba umechagua hiyo issue, so fine we endelea’. Basi nikajaribisha kuongea naye lakini hakuweza kunisikiliza lakini luckily the next day wakati ndio nashiriki nimekaa pale time ya kujibu swali namuona pale anapiga picha kwahiyo he was there na alinisupport mpaka nilipofika Miss Tanzania lakini after that sababu nilikuwa ambassador wa Vodacom nikawa nafanya kazi Vodacom nikawa sionani naye vile kama kawaida, kila akinipigia simu nipo busy, yeye mwenyewe akasema tu ‘bwana mimi siwezi’. Basi tulielewana vizuri na mpaka kesho tunaongea, tunasalimiana’ 
_DSC1055 copy
Uwewahi kusema bila Kanumba usingeingia kwenye movies, marehemu alikuwa ana mchango gani kwako?
Nakumbuka nilipokutana na marehemu nilikuwa niko na dada yangu mimi nilikuwa nakaa na dada yangu, kwasababu once nilishawahi kuishi na mama yangu and then from there unajua baada ya kuingia kwenye nini nini nikawa busy. Dada yangu mimi kaolewa lakini kwa dada yangu nilikawa nahisi kama pako free zaidi, kwamba mama ukirudi ‘umetoka wapi sijui nini na nini hivyo, alikuwa haelewi. So ikabidi tu nianze kuishi na dada yangu.
Kwahiyo dada yangu akawa ananielewa, kwasababu hayupo sana protective kama mama. Siku hiyo tunabadilisha seating arrangement ya pale nyumbani kwa dada yangu tukawa tunatafuta carpet like different furnitures, so tukawa tumeenda hapa kulikuwa na hili duka kubwa hivi la Mwanamboka kulikuwa kuna furniture center, Pentagon, so tukawa tumeenda pale wakati tunaenda tulimkuta Kanumba wapo nje wameweka makamera yao nini ,wanashoot Lost Twins. So sisi tumeingia tunaona tu makamera, tumepark gari tumeingia ndani tunaangalia furniture. Akatokea Maya tukasalimiana akaniambia, ‘ jamani nakupenda’ na mimi nikamwambia na mimi napenda unavyoigiza’ nini na nini.
Tukatoka nje tukakutana tena na Maya akaniambia ‘jamani jamani kama unaweza pita kidogo tu hata uonekane, hata usalimie’.
Nikamwambia siwezi kwasababu nipo kwenye mkataba, akina Uncle Hashimu wataniua wakiniona nimefanya kazi au nimetokea kwenye nini bila kuwaconsult so akaniambia ‘basi sawa tuachie namba yako’. Wakati ananiambia tuachie nambo yako, Kanumba huyo anapita, ‘Kaka kaka ngoja umemuona Wema?’ Aliniringia sana.
‘Mambo’ nikamwambia ‘fresh vipi’ ‘safi’ nikamwambia poa,’Kaka basi chukua namba yake ya simu tunaweza baadaye like tunaweza tukamtumia kwenye movies’, ,Kanumba akamwambia achukue simu yake ndani. Basi nikamwangalia mimi mwenyewe basi ndio ninamwona mara ya kwanza, ‘Hee Kanumba’, kwasababu nimeangalia sana michezo yao. 
Basi, so baada ya hapo akaleta akachukua namba yangu akanibeep nikamsave, basi mimi nikaondoka zangu. Sijafika mbali naona namba inanipigia ambayo nimeisave vilevile Steven Kanumba, nikapokea ‘Hello’ akaniambia ‘vipi, safi Kanumba hapa’ nikamwambia ‘namba yako nimeisave’ ‘haya basi sawa basi baadae’ nikamwambia ‘poa’.
Mara like jioni jioni hivi akaanza kunitext ‘mambo’ ‘Safi’ ‘vipi uko wapi?. Basi kila siku tukawa tumejengeana tabia ya kutextiana kila siku tunandelea for one weak tunatext mara yeye ataniuliza umekula nini, mara sijui nini, obvious kwa mwanamke unakua tu unajua kwamba mwanaume akiwa ana interest na wewe. Kidogo tukaanza kuulizana una boyfriend una girlfriend sijui nini, hivyo. Akaniambia mimi ‘nipo kambini Lamada’ akanielekeza nikafika.
Basi nimefika siku hiyo tumekaa pale garden akaniambia ananipenda na nini, hivyo. Kipindi hicho nilikuwa sina boyfriend nilikuwa very very single, so nikamdanganya nikamwambia ‘mimi na boyfriend wangu sijui nini’ akaniambia ‘naomba tu just like nifikirie basi’ Nakumbuka tulivyokuwa tunaondoka ndo tukakiss, it was our first kiss. Basi nikaondoka, akaniambia ‘unaweza kurudi tena nikamwambia siwezi akaniambia please, please naomba urudi tena unikiss’ nikamwambia ‘sawa’ basi nikarudi then akaniambia ‘l love you, love you too, mapenzi yakaanza.
Basi kwenye mapenzi yetu ndo akaniambia like ‘nataka kuact movies na wewe’ nikamwambia ‘mimi siwezi kuact’ akaniambia ‘mimi nahisi unaweza kuact hujajua tu’ nikamwabia sijawai kufikiria kuact, akaniambia ‘unaweza kulia’, nikamwambia ‘nilie nina sababu gani ya kulia’ akaniambia ‘basi kama huwezi kulia tutakumenyea vitunguu, ‘vitunguu ukimenya si unalia, basi tutakuwa tuna kumenyea vitunguu’ .
Akaniambia niende kuonana na bosi wake. Nilivyofika tu ofisini nikaonana na Mtitu Game. Akanipa script akaniambia nikasome kama story akaniambia ‘wakati unasoma uwe unasoma sana concentrate kwenye Dina. Basi vile tukiwa tukikutana tunafanya mazoezi nini, akaniambia ‘sawa basi wewe you are ready to shoot. Nilivyo shoot movie yangu kwanza, hauwezi amini, I just felt yaani kwanza niliona iko very easy. Kwa wengine wanaona it’s hard unajua.
Baada ya hapo ndo nilikuwa tayari nimetoa taji, I had to go back to school. Nikasafiri nikaelekea Malaysia kufanya kozi yangu ya mwaka ya International Business, wakati niko Malaysia nikatumiwa movie yangu ya Point of No Return. Tumekaa tunaangalia na marafiki zangu nikaona kwamba kumbe it’s nice, it’s fun. Nikampigia simu, ‘narudi for likizo soon naomba uniandalie script nataka ni shoot movie nyingine’
Nimerudi kweli ndo tukashoot Red Valentine, Family Tears, White Maria yaani tukashoot movie movie nyingi hivi so from there nikawa nimeshajikuta katika movie, so that why I keep saying kwamba without him nisingejua.
_DSC1040 copy 
Hebu tuzungumzie uhusiano wako na Diamond ambao katika mahusiano yako yote ndio ulioandikwa zaidi kwenye magazeti, unakumbuka mlikutana wapi?

Mi na Diamond tuliwahi kukutana mara moja tu Billcanaz na hatukuwahi kusalimiana kabla ya kuanza uhusiano lakini tulikuwa tunaangalia sana, so nakumbuka alikuwa yupo smoking room kwahiyo tukawa tumepeana migongo, nilikuwa na rafiki zangu wawili. Nikamuona akaniona yeye alikuwa na rafiki yake, hatujasaliamija hatujafanya chochote mimi nimechukua vinywaji tukatoka nje na marafiki zangu tumesimama hapo nje nikawa naambiwa ‘yule ndio ameimba Kamwambie’ kipindi hicho nilikuwa namuona wa ajabu sana ila tu alijiseksisha kiasi fulani (kicheko kirefu).
Kipindi hicho mimi nilikuwa natoka na Chaz Baba so nakumbuka hiyo ndio ilikuwa the first and last day tumeonana. Mimi nikasafiri nikaenda Marekani, nilipofika kipindi hicho Kamwambie ndio ilikuwa hot na Mbagala ndio karelease. Dada zangu walikuwa wanampenda sana Diamond yaani just from the songs. Dada yangu wa kwanza ana miaka 14 yupo Marekani na hajawahi kurudi Bongo toka aondoke kwahiyo alikuwa anaona Bongo inafanya vizuri sasa hivi akaniuliza kama tuna urafiki na Diamond nikasema sio sana tunajuana tu. 
Akaniambia nimwambia aende Marekani kufanya show sababu kila party tuliyokuwa tunaenda lazima watapiga Kamwambie halafu kila mtu anaipenda. So watu wakaanza kuniambia like ‘hebu find contact naye huku kuna mapromoter aje kufanya show’na kipindi hicho Profesa ndio alikuwa amekuja nikamwambia basi sawa mi nitamtafuta.
Nikamwabia Da Rehema, Ray C anitafutie contact zake. So siku moja nikaona anaplan kwenda kufanya show London, nika mclick Diamond Platnumz nikamtext, nikamwambia ‘hey mambo vp mzima upo London’ akaniambia ‘No mamie sipo London sijui ni nini’ nikamwabia ‘anyways Wema hapa nipo Marekani halafu it happens una fans wengi, akaniambia basi sawa acha nimalize issue ya London halafu nitakuambia. 
Basi tukajenga tu mazoea tukawa tunachat nini yaani ikawa yeye anaingia Facebook kuchat na mimi naingia kuchat naye, washkaji tu yaani. Akawa ananiambia ‘bado uko na Chaz na nini’ nikamwambia yeah nipo na Chaz. Sasa ilikuwa ni kama mwezi wa nane wa tisa kama sikosei. Mimi wakati nipo Marekani nilikuwa naambiwa sana news kuhusu Chaz, mara Chaz sijui yupo na mwanamke gani, hiyo hiyo Facebook watu wananitumia mpaka picha nikumuuliza anakataa.
Sasa mimi nakumbuka dada yangu alikuwa anampenda sana Chaz so siku ya siku amekutana naye yupo sijui na mwanamke gani alipoaniambia nikasema, basi. So nikajikuta namuelezea matatizo Diamond. Siku niliyoamua kabisa mimi and Chaz are done nikamwambia mimi siwezi. So tukawa tunawasiliana na Naseeb hivyo. Siku moja tukanuniana, alikuwa amealikwa Ikulu halafu nikawa namtext hajibu, nikimpigia simu hapokei akaja akatoka akanipigia simu nikawa sijibu. Akanitumia meseji ‘baby I am sorry, we ndio faraja yangu sijui ni nini…. I LOVE YOU. Sikuona kitu kingine chochote nikaona tu hiyo. Basi nami nikamjibu sawa nimekusamehe lakini sijakusamehe sana, nimekusame kidogo. Akaniambia ‘niambie kitu kizuri’ na mimi nikamwambia I LOVE YOU. Basi akaniambia ‘mwenzio nakupenda, nachanganyikiwa’ basi no mapenzi yakaanza hapo.So niliporudi kutoka Marekani mimi na Naseeb tukaanza kuishi pamoja. 
_DSC1061 copy
Mwaka jana alipooenda kutumbuiza kwenye Big Brother Africa, alidai kuwa ameweza kuongea Kiingereza kwasababu yako, ulikuwa ukimfundisha ama ulikuwa ukipenda kumuongelesha Kiingereza zaidi?
Yes. Naseeb alikuwa hajui Kiingereza, alikuwa anajua cha juu juu. Ila mimi na Naseeb tumekaa pamoja mwaka mzima kama mke na mume. So mimi nilivyo kidogo nimetupia Kiingereza kwahiyo hiyo ilikuwa inampa tabu kwenye the first two months kwahiyo most of the times nikawa naongea naye Kiingereza. Lakini he is smart, Naseeb is very smart yaani akiwa haelewi kitu ‘hivi baby hapa kwenye has na have unafanya nini, hapa natumia tense gani? Niweke ing niweke nini?’ mwisho wa siku nikajikuta like tunatumia most of the time kufundishana. Akisema kitu ambacho sicho namwambia ‘usije ukarudia tena kusema hivyo mbele za watu watakucheka’. So akajikuta tu anaweza.
Kwanini mliachana?
Mimi na Naseeb tuliachana baada ya yeye kunicheat na Jokate .Nilikuwa sijui and maisha yangu yote tangia nimeanza mapenzi na Naseeb naweza kusema kuwa sikuwahi kuwa unfaithful. I used to be very faithful to him na tulikuwa tunapendana sana. With Naseeb nilikuwa nimesharidhika na maisha ambayo niko nayo na hata kama yalikuwa not good, whatever lakini tayari nilikuwa nipo satisfied with me and him nilikuwa tayari nimesharidhika naye. 
Nadhani pia inacost mwanaume akishajua kwamba anakutawala in one way or another so labda ni shetani au ni ibilisi alimuingilia baada ya kutaka kuanza kushoot video ya Mawazo ndo rumors zilianza, nikawa siamini kwanza. Siku moja ndio nikapigiwa simu na rafiki yangu anafanya kazi Piccolo akaniambia ‘Diamond yuko hapa na Jokate na wanakiss’. Nilitoka, nikachukua taxi nikaenda mpaka Piccolo, kitu cha kwanza niliona gari yake. Nilivyofika nikawakuta sijui wamewekeana miguu. Nilivyofika pale nikawasalimia wakawa wako kimya na nimeona ile kitu nikawaaga nikaondoka zangu. Nikaliaaaa, amerudi wakati huo bado tunaishi pamoja akanikutana napanga nguo, hakutaka kuongea sikutaka kuongea, tukachuniana, sikulala mimi na Naseeb kitandani for one week. Anaiona ile hali lakini hataki kuanza. Nikachoka, nikaja tu siku nimepanga nguo zangu nikaenda kwa dada yangu ndio ikawa kimoja. Basi mimi nikamwacha akaendelea na maisha yake na mimi nikaendelea na maisha yangu. 
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

42 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nani ana shida ya kukufahamu?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwani ulitumwa usome...sio kila liandikwalo lazima wote tusome ungepita tu.....lione kwanza msura umekusinyaa kama m....b..o iliyomaliza kazi...!

      Delete
    2. Hahahaaa. Mdau mbavu zangu. Wa2 mna maneno ya ghaflaghafla kweli hicho kipaj. Thnx mdau 4 making ma night.

      Delete
    3. Sawa huna shida ya kumfahamu,kwani katuma usome?????hebu nenda kameze Bitter pill upumzike maana kwa Wema ndo kwanza mkoko unatoa maua...

      Delete
    4. ningekuwa mimi nisingecoment coz she iz most liked

      Delete
  2. waliomuuliza na wakaeka hpa historia yke na sie tuliosoma ndo tuliokuwa na shida ya kumfahamu we km huna shida hyo umesoma ya nin pimbi wee,kafie mbali uko

    ReplyDelete
  3. Jokate mwiz wa waume kama penseli

    ReplyDelete
  4. Inaonyesha boy wako wa kishule-shule ulimwaga baada ya kupata taji la mis tz,si ndo zenu nyie madem.

    ReplyDelete
  5. I love u r love diamond jani. Ila jokate nae shetani kweli. Paka jike yule

    ReplyDelete
  6. Nimeipenda sana. Lyf has hills and slopes jus work harder bby gal.

    ReplyDelete
  7. Waoooo ni twins na my hubby GODWN naye kazaliwa keo, its me JACKY ARUSHA

    ReplyDelete
  8. WEMA N DIOMOND ARE FOREVER km hutak kufaaaaaaaa

    ReplyDelete
  9. We love u Wema no matter what pple sayyyyyyyyyy........

    ReplyDelete
  10. Huyo wa kwanza aliye comment ana joto hasira atakuwa penny. Poyeee bibi tarabushi

    ReplyDelete
  11. Yani kama kweli Jokate alimfanyia mwenzie hivyo...Kweli huyo demu atakuwa na malaya alichafuka yadi kakosa mwanamme wake mwenyewe. Sasa baada ya kuwa na Diamond ndo amepata nini...Loh!Jokate utakuwa na balaa ndugu kwasababu yadi Dimondo amekuacha..Lol utakuwa tu mzuri wa kuchezewa sio kuwekwa ndani kama mke. Acha kuwa fake...Na acha umalaya na kuchukua mabwana za watu..Utakuja kupigwa laana za ajabu ujute maisha shauri yako.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umenena mdau!!malipo hapa hapa ka Jokate kaliachwaje gafla sasa hahahaaaaaaa afu Diamond akarudi kule kule kwa Wema...

      Delete
  12. Ila uongo dhambi diamond na wema kapo yao ilikua nzurisana sijui kama itakuja tokea tena!I wish mrusiane!

    ReplyDelete
  13. kumbe Joketi ndo mbaya dah! Nakuchukia sana kuanzia leo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ulikuwa hujui hilo??Diamond alimuomba kwa uzuri tu washoot video ya mawazo,hapo ndo kakajitongozesha mazima na si unajua Dimondo hacheleweshi akakafyatuaaaa...lkn baadae alikaacha bila hata taarifa akamrudia Wema...

      Delete
  14. xafar ya mapenz inaytaj patience,understandn,4gvin each other!no one z perfekt!kusema kwel,wema&plutnumz walimatch xn,ila bas wa kuyatengeneza au kuyaharb ni wao,yetu maoni tu.

    ReplyDelete
  15. One sentence,lov u wema

    ReplyDelete
  16. Wow,inasisimua.keep going dia

    ReplyDelete
  17. Mbona wema hujaendelea kidogo? Kuna ki2 nilitaka kukisoma hapo baada ya D'mon, c unajua wambea tena?

    ReplyDelete
  18. Hapo sioni mjanja, siku zote wajanja ni wale wanaomrudia Mungu. Nashangaa watu mnapoteza muda wenu kushabikia upuuzi unaofanywa na hao jamaa! Hebu tuwakosoe ili wamrudie Mungu. Hapo tutakuwa tumefanya jambo la msingi kuliko yote duniani. Hivi sasa tunachokifanya ni kuzidi kuwapotosha. I tell u my dears we will b answerable at the dooms day.

    ReplyDelete
  19. Ona akina Masanja, hivi sasa ni wahubiri hao ndiyo wajanja, siyo hao akina D & W wanaojivunia kufanya zinaa huo si ujanja bali ni ushamba,.

    ReplyDelete
  20. Ndio jaman na wema akipenda anaonekana anapenda kan, co relation yke inakua public I lov wema ni vle anajulikana tu ndo maana anaonekana ajatulia bt ts normal things

    ReplyDelete
  21. Eeeehh na ww hapo juu c uwashauri wamrudie Mungu umekatazwa kwanii mxiuuu unamlaumu nan sasa humu we mjuc

    ReplyDelete
  22. Hilo lijokate ndo maana diamond alilibwaga bila sababu yoyote chezea karma wewe karma is a big bitch just like jokate alifikiri yeye ndo atatafuna pesa za diamond mi nawaambia bora ya wema kila analofanya liko wazi joketi mambo yake ya gizani ni machafu ukilinganisha na wema wema ni saint kwa jokate

    ReplyDelete
  23. Hahahahaaa umenifurahisha mdau hapo juu

    ReplyDelete
  24. Hapana Wema katuficha yeye ndie alie anza kumcheat Diamond asimsingizie Jokate Wema ndio mbaya lkn nampenda ata Jokate pia

    ReplyDelete
  25. ukwel wanaujua wenyewe,2ombeane uzma..happy bdai wema

    ReplyDelete
  26. ukwel wanaujua wenyewe,2ombeane uzma..happy bdai wema

    ReplyDelete
  27. C kweli,yule almas alitaka tu kujua haka ka malaya jokeri ka koje bila plan ndo maana,wema alitulia kwa almas for sure ila tu almas ulimbuken ulimponza.ila tuachen utani joket ni whore ila hajulikan sabab ya kasura ka upole,ila ni beautful whore.

    ReplyDelete
  28. Tunashukuru kwa kupata kujua ABCs za maisha ya mrembo Wema maana tumezoea kusikia habari za magazetini tu. Safari ya mapenzi ni ndefu jamani na mtu huwezi kujilazimisha kukaa na mtu ambaye anacheat, hata kama ni wewe lazima utaamua kujitoa tu, so ni kawaida. wengine wanaseme eti mtu anabadilisha wanaume sasa ufanyeje kama patner wako sio mwaminifu? Kila la heri wema ipo siku itampata wako wa maisha. Ila usigombane na mama yako sababu ya wanaume maana wao ni wa kupita tu! Nachukia sana wanawake wanaopora wapenzi wa wenzao, yani akipata chance , atajirahisisha mpaka atoe k ndio anaona raha. kiukweli pea yako na diamond ilikiwa juu sana , yani mnapendeza na kupendana, i hope ipo siku mtarudiana na almasi atatulia nawewe!

    ReplyDelete
  29. I love u Wema kuwa na msimamo uheshimike pia angalia wanaume wengi hawajiheshimu wanataka umaarufu tu wakutembea ovyo na wanawake nakupa bigup

    ReplyDelete
  30. Diamond nakushauri tu, rudi kwa Wema jamani.... pia najua bado unampenda, huko kwa pensel unajikaza tu. hata baby zenu hazinogi. yani siku ukirudi kwa wema then fanya shoo moja uwanja wa taifa hakuna ataekosa. DIAMOND AND WEMA ARE FOREVERRRRR

    ReplyDelete
  31. Sasa mbona Mange anajishaua ye ndo alimshawishi hadi akawa anakesha home kwao...while there was no kipingamizi..hiz chai hizi!!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. mmh mdua bora ulivoniwahi!!mweeh mange kajisemesha hadi povu likamtoka! kumbe alikua anatudanganya? eti anakiesha na kushnda kwao mpaka akampromise mama wema kuwa lazima wema ashinde,,,mweeh!! AIBU

      Delete
  32. DAH..!AMENIFURAHISHA HUYO ALIYEMTUKANA MWENZAKE ....................Kwani ulitumwa usome...sio kila liandikwalo lazima wote tusome ungepita tu.....lione kwanza msura umekusinyaa kama m....b..o iliyomaliza kazi...!....DAH..!KARIBU NUSU SAA NZIMA NACHEKA TUHILI TUSI NA KILA NIKIKUMBUKA NACHEKA TU NATAMANI NIMU9NE MMMH!

    ReplyDelete
  33. N a nyie mnaotaka ulokole mnaingia kusoma haya ya nini jamani msiharibu mapozi ya watu?mimi pia nilikuwa naipenda sana hiyo couple ya wema na diamond na huyo aliyewavuruga basi amsamehe haikuwa riziki yake atampata wake wa maisha..............

    ReplyDelete
  34. wema forever and for always burundi tunakupenda sanaaaaaaaaa

    ReplyDelete

Top Post Ad